Wakurugenzi wawekwa kitanzini
Amesema suala la kila Halmashauri
kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na
vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima na
si hiari.
Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema
hayo leo (10 Aprili, 2016) alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na
wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema
ambako lifanya mikutano ya hadhara.
“Halmashauri ambayo itashindwa
kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano
kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safariiri,”
amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.
Waziri Mkuu, Majaliwa yupo
wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi inayolenga kukagua
shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri
nchini kutimiza wajibu wao na serikali haitamvumilia yeyote
atakayeshindwa.
Pia Waziri Mkuu, Majaliwa
amewataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili
zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk.
John Magufuli waweze kunufaika.
Amesema fedha hizo ambazo
zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi
mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka
watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika
vikundi.
Katika hatua nyingine Waziri
Mkuu, Majaliwa amesema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la
korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie
mfumo wa Stakabadhi ghalani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni