Uchukuzi Sports Club, yajifua sawasawa kwa ajili ya mashindano ya Mei Mosi huko Dodoma
Na Raymond Urio
Timu ya soka ya Uchukuzi
Sports Club iliyopo chini ya Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano
ikifanya mazoezi wakijiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi
Wachezaji wa Uchukuzi Sports
Club wakifanya mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi kwenye
uwanja wa soka uliopo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA).
Akimama wa klabu ya Uchukuzi wakifanya mazoezi kabla ya kuvuta kamba.
Wachezaji wa timu ya wanawake ya kuvuta kamba ikiwa kwenye mazoezi katika viwanja vya JNIA.
Kikosi kabambe cha timu ya soka ya Uchukuzi kikiwa pamoja na kocha na meneja wa timu hiyo Robert Damiani (kushoto).
………………………………………………………………………………………….
TIMU ya Uchukuzi Sports Club
imepania kufanya vyema kwenye mashindano ya Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei
Mosi) yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 16 mwaka huu.
Mwenyekiti wa timu hiyo
inayoundwa na wafanyakazi wa taasisi zinazounda Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mohamed Ally alisema kuwa timu yake itafanya
vizuri katika mashindano hayo, kutokana na maandalizi kabambe
waliyofanya.
Ally alisema kuwa kwa sasa wako
katika mazoezi makali kujiandaa na mashindano hayo, ambayo yatafikia
kilele siku ya Mei Mosi mjini Dodoma.
Ally alisema Uchukuzi Sports Club
inaundwa na timu za michezo ya soka, netiboli, kuvuta kamba, bao,
karata, riadha, baiskeli na vishale.
Alisema kuwa wana uhakika timu
yao kufanya vizuri katika mashindano hayo, kutokana na kufanya mazoezi
kwa muda mrefu chini ya makocha wazoefu wa michezo hiyo.
Ally aliwataja baadhi ya makocha
hao kwa upande wa soka kuwa ni pamoja na Kenny Mwaisabula, Robert
Damian, Terry, Kingsley Malwilo na Abunu Issa, ambao wameifanya timu yao
kuwa tishio kwa timu zingine, wakati netiboli inafundishwa na mchezaji
mkongwe Judith Ilunda.
Alisema kuwa timu zao hizo
zimekuwa zikicheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali, ili kuwawezesha
makocha kubaini makosa na kufanya marekebisho ya mwisho kabla timu hiyo
haijaondoka kwenda Dodoma.
Naye Meneja wa Uchukuzi Sports
Club, Robert Damiani alisema kuwa timu yao inatarajia kwenda Dodoma
Aprili 14 tayari kwa mashindano hayo.
Damiani alisema wanauhakika wa
kufanya vizuri na kuvunja rekodi ya mwaka jana ya kutwaa vikombe 13,
kati ya hivyo vitano vikiwa ni vya ushindi wa kwanza, wakati
vilivyosalia walishika nafasi ya pili na tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni