TIMU ZOTE ZILIZOTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, KILA MOJA IMESHINDA KWA 3-2
Umeona timu nne zilizovuka na kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kila moja ilishinda kwa jumla ya mabao 3-2.
Tuanza
na Real Madrid, mechi ya kwanza ilifungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya
Wolfsburg ya Ujerumani. Mechi ya pili mjini Madrid ikashinda kwa mabao
3-0 na kufanya jumla iwe 3-2.
Atletico Madrid ikiwa ugenini, ikapoteza kwa mabao 2-1 lakini nyumbani, ikashinda kwa mabao 2-0. Jumla ikawa 3-2.
Manchester
City ikiwa ugenini Paris, ikapambana na kupata sare ya mabao 2-2.
Iliporejea England, ikashinda 1-0 dhidi ya PSG. Jumla ikawa mabao 3-2.
Bayern
Munich wao walianza kushinda nyumbani kwa bao moja, lakini waliposafiri
kwenda Ureno kuwafuata Benfica, matokeo yakawa sare ya 2-2. Jumla ni
mabao 3-2, Bayern wakisonga mbele.
Itakuwaje kwenye hatua hiyo ngumu. Kwanza tusubiri droo itakayopangwa kesho, nani atacheza dhidi ya nani..

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni