Mchezaji
wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es
Salaam jana usiku kwa mwaliko wa siku tano wa Kampuni ya Vizimbuzi ya
StarTimes.
Staa wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu alipokuwa akiwasili Uwanja wa Ndege.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Be. Lanfang Liao (kulia),
akimuelekeza jambo mchezaji huyo wakati wakielekea kupanda gari kuelekea
Hoteli ya Serena. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa
StarTimes Tanzania, William Masy.
…………………………………………………………………………………………………………………….
KAMPUNI
inayojihusisha na utoaji wa huduma za matangazo ya luninga kwa njia ya
dijitali, StarTimes Tanzania imepokea ugeni mzito wa aliyekuwa mchezaji
nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Bw.
Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa kampuni hiyo kwa bara la
Afrika ambamo imo kwenye takribani nchi zaidi ya 10.
Akizungumza mara baada ya kutua
kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jana usiku,
mchezaji Nwankwo Kanu alisema kuwa anajisikia furaha kubwa kuwasili
Tanzania salama kujumuika na kmapuni ya StarTimes katika shughuli
mbalimbali kwa ndani ya kipindi cha siku tano atakazokuwepo.
‘’StarTimes ni kampuni kubwa
barani Afrika na imeleta mapinduzi makubwa katika upande wa matangazo
ya luninga kwa dijitali kwani imeweza kutoa huduma zake kwa ubora mkubwa
na gharama nafuu ambazo kila mtu anaweza kuzimudu.’’
Kwa upande wa vipindi na
chaneli za michezo mchezaji Kanu amebainisha kuwa kampuni ya StarTimes
imepiga hatua kubwa hasa kwa upande wa kupata na kuonyesha michezo ya
ligi ya soka kubwa barani Ulaya kama vile za Bundesliga na Serie A za
Ujerumani na Italia.
“Mimi kama balozi wa StarTimes
barani Afrika nitajitahidi kawa kadiri ya uwezo wangu kuwa kiungo muhimu
katika kuhakikisha ninaiwakilisha vema kwa wateja wake, hususani katika
shughuli mbalimbali kama vile soka kama mjuavyo ni mchezo unaopendwa na
watu wengi duniani na hata miongoni mwa waafrika wenyewe.” Aliongezea
Kanu.
“Hivyo basi kwa muda wote
nitakaokuwepo nchini Tanzania nitashirikiana na StarTimes kwa ukaribu
katika shughuli za kikampuni na pia za kijamii kama vile za kielimu na
afya. Kama mjuavyo katika mahala popote unapofanyia shughuli zako ni
muhimu sana kuijali jamii inayokuzunguka kwani yenyewe ndiyo sababu
kubwa ya wewe kuwepo.” Alihitimisha
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes
nchini, Bw. Lanfang Liao amesema kuwa, “Uwepo wa Kanu Tanzania ni fursa
ya kipekee na pia ni moja ya jitihada kubwa za kampuni yake katika
kuimarisha na kuhudumia wateja wao hususani kwa vipindi vya michezo na
burudani na ninaamini uwepo wake utaleta chachu kwetu sisi na wateja kwa
ujumla.”
“Nwankwo Kanu alikuwa ni
mchezaji wa kimataifa si tu aliiwakilisha nchi yake ya Nigeria kimatifa
katika michuano mbalimbali lakini pia alifungua milango kwa vipaji vya
Afrika barani Ulaya. Hivyo basi tunaamini bado ni maarufu na ana heshima
kubwa miongoni mwa watanzania na wapenda soka barani Afrika. Kwa yeye
kuwa balozi wetu ninaamini tutafaidika kwa namna gani tuboreshe huduma
zetu ili kuiteka mioyo ya watanzania na waafrika kiujumla.” Alimalizia
Bw. Liao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni