Ijumaa, 1 Aprili 2016

SHIRIKA LA POSTA KUZINDUA HUDUMA MPYA YA "POSTA MLANGONI" APRILL 5 MWAKA HUU



NA RAYMOND URIO, Dar
KATIKA Kuhakikisha kuwa Shirika la Posta Tanzania linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za serikali ya awamu ya Tano za kuleta maendeleo ya haraka kwa mwanachi, shirika hili kuanzia jumanne litaanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani ya nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani.


 
  Kaimu Poster Master Mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga akizungumza jana na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani), kwenye ukumbi za Ofisi hizo, kuhusiana na shirika hilo kufungua huduma ya "Posta Mlangoni" huduma hiyo itazinduliwa Aprill 5 mwaka huu, kushoto ni Meneja mkuu wa rasilimali za shirika la Posta Tanzania, James Sando.
 
Huduma hii inayojulikana kama “Posta Mlangoni” itaanza katika baadhi ya kata za hapa jijini Dar es Salaam, Arusha na Dodoma inaboresha ile iliyokuwapo tangu enzi za ukoloni ya masanduku yaliyoko Ofisini za Posta ambayo mtumiwa nanlazimika kufuata yeye mwenyewe barua, vifurushi, taarifa au bidhaa aluizotumiwa kupitia Ofisi za Posta.
Serikali kupitia Ofisi ya Raisi ( TAMISEMI ) tayari imeweka miundombinu hiyo katika kata 8 za jiji la Arusha, kata 8 za manispaa ya Dodoma na kata 32 kwa jiji la Dar es Salaam. Miundombinu hiyo ni mitaa kuwekewa nguzo za kuonesha jina la mtaaa, nyumba zilizopo kwenye mtaa huo kuwekewa nambari za kiposta.
Baada ya kuznzisha huduma hii jumanne ijayo hapa Dar es Salaam, Arusha na Dodoma ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2015 na 2016, awamu ya pili itakayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016 na 2017 itahusu mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Pwani, Manyara, Simiyu na Geita pamoja na Tanznia visiwani( Unguja na Pemba).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa ofisi hizo, Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Fortunatus Kapinga, alisema kuwa Huduma hii ni msukumo mpya wa ndani ya shirika wa kuhakikisha kuwa yanakuweko mabadiliko katika uendeshaji na utoaji wa huduma za mawasiliano ya Posta nchini ili kukabiliana na kasi ya teknolojia, kukidhi mahitaji ya soko, kuboresha maisha ya wananchi na kufanya Tanzania kuwa kinara wa hudumabora za mawasiliano.
“Kupitia huduma hii yamefanyika mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji katika baadhi ya Ofisi ili kuhakikisha kuwa uchambuzi wa barua unafanyika kwa uhakika zaidi, anwanwi zitatambuliwa ili kuongeza kasi ya kusafirisha na kusambaza barua,
“Aidha kipindi hiki cha mpito ambapo hapo baadae ndani ya kipindi cha miaka mitatu shirika litasambaza huduma ya “Posta Mlangoni” nchi nzima,” alisema Kapinga.
Hata hivyo Kapinga alisema kuwa huduma hii imeanzishwa sasa kutokana na jitihada zax serikali kuweka miundombinu ya Anwani za Makazi na Postikodi kupitia wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini ( TCRA) na wadau wengine.
“ Miundombinu hii ni pamoja na barabara na Mtaa kuperwa majina yanayosomeka kwenye nguzo zilizosimikwa pamoja nanyumba kupewa majina yanasomeka  kwenye nguzo zilizo simikwa na nyumba zilizo pewa namba,” alisema Kapinga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni