POLISI: UHAKIKI WA SILAHA KUENDELEA MIKOA YOTE,
BAADA ya wakazi ya jiji la Dar es Salaam kuanza
usajili wa kuhakiki Silaha Jeshi la Polisi nchini limetoa miezi mitatu kwa
mikoa mengine nchini kwa wamiliki wote
kufanya uhakiki wa silaha la sivyo sheria itachukua mkondo wake.
Akizungumza
jijini hapa jana, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Nsato Malijani, alisema
wananchi wamejitokeza kusajili na kuhakiki silaha zao ambapo rais Dk John
Magufuli alikuwa wa kwanza kufanya hivyo na kwamba hali ya uhalifu wa makundi
bado ipo, kuwataka wananchi wananchi kutoa taarifa endapo wakibainika makundi
wanaojihusisha na uhalifu na yenye silaha.
Kamishina wa oparesheni na mafunzo wa makao mkuu ya jeshi la polisi, Nsato Mssanzya akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani), kuhusiana na jeshi la polisi nchini kutoa linatoa muda wa miezi mitatau kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kuhakiki silaha kwa nchi nzima.
Kamishina Malijani alisema uamuzi wa kutoa muda huo
katika mikoa iliyobaki ni kutokana na kwamba awali walitoa muda mchache hali ambayo ilisababisha msongamano
katika vituo vya polisi.
Alisema hali
hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa mchakato huo kutofanyika kwa haraka jambo
ambalo limekuwa kero na kuleta mkanganyiko kwa wamiliki pamoja na kupunguza
hali ya usalama katika vituo vya polisi.
"Hivyo
ni imani yangu kwamba muda huo utatosha kwani utatoa nafasi kwa watu ambao
hawajalipia ada ya umiliki wa silaha zao kulipia na kusajili pamoja na kuondoa
msongamano wa watu katika vituo vya polisi waliojitokeza kwaajili ya kusajili
silaha zao," alisema.
Alisema jeshi
hilo halikuweka wazi idadi kamili ya sialaha ambazo hazikulipiwa na kiwango
chake na kuweka wazi kuwa jambo hilo litaelezwa mara baada ya kukamilika kwa
mchakato huo na kukusanya taarifa kutoka katika mikoa yote nchini.
Alisema hali ondoa msongamano wa watu katika vituo
vya polisi waliojitokeza kwaajili ya kusajili silaha zao," alisema.
Akizungumzia uhalifu na ukamataji wa silaha,alisema
hivi karibuni jeshi hilo limefanikiwa kukamata watu katika maeneo mbalimbali
wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado wanaendelea kufanyiwa
uchunguzi.
"Watu hawa wamekamatwa Mafia, jeshi
linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili tuweze kupata taarifa mbalimbali na kuweza
kuwatia
nguvuni wengine ili tutokomeze kabisa suala la
uhalifu nchini," alisema
Alisema wanaendelea
kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa
na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili uwakamata watu hao.
"Jeshi kama jeshi pekeake haliwezi
likakakamata wahalifu wote bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao
wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili
waweze kukamatwa," alisema Malijani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni