MAYANJA ANA IMANI KUBWA KIKOSI CHAKE KITAFANYA KWELI DHIDI YA TOTO LEO
By Newsroom on April 17, 2016
Kocha
Jackson Mayanga ana imani na maandalizi ya kikosi chake kuwa kina uwezo
mkubwa kuwa kitaishinda Toto African kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam, leo.
Hata hivyo, Mayanja anajua mechi yao hiyo ya leo itakuwa ni ngumu kwa kuwa Toto wangependa kushinda pia.
Katika
mechi ya mzunguko wa timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba huku Toto wakisawazisha bao katika dakika ya mwisho
kabisa.
Mayanja amesema wamejiandaa vizuri na kinachotakiwa ni kucheza kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kutumia nafasi.
"Kwenye
mpira ukiwa makini unafanikiwa, ukikosea ujue utaadhibiwa. Sisi
tumejiandaa vizuri na tunataka kucheza vizuri na kushinda.
"Wachezaji
wangu wanataka kushinda, hivyo litakuwa ni jambo zuri tukiingia na
kupambana kwa asilimia mia tukiwa makini," alisema.
Simba
inarudi uwanjani leo katika mechi ya Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza
mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union. Ilifungwa
mabao 2-1 na kung'olewa katika hatua ya robo fainali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni