Jumapili, 3 Aprili 2016



   DENIS RICHARD NAE AFUNGIWA MIAKA 10
 
 
Kipa  wa zamani wa Klabu ya Simba, Denis Richard kinda wanaochipukia, amefungiwa miaka 10 na kutakiwa kutoa faini ya Sh milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kupanga matokeo.

Richard sasa ni kipa wa Geita Gold Mine na amefungiwa baada ya kwenda chooni kwa zaidi ya dakika 15 wakati Geita ikiwa inaivaa JKT Kanembwa katika mechi ya mwisho ya Ligi Daraja la Kwanza wakati mechi ilipoisha kwa Geita kuitwanga Kanembwa kwa mabao 8-0 na kufanikiwa kupanda daraja, yaani Ligi Kuu Bara.

Lakini Richard amepatikana na hatia kwa kuwa alichelewesha mpira kuendelea ili mechi nyingine ya kundi hilo iliyotakiwa kwisha sawa kati ya Polisi Tabora Vs JKT Oljoro iliyokuwa inachezwa mjini Tabora.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni