Jumapili, 3 Aprili 2016

 

 

Wakili Jerome Msemwa  ambaye ni Makamu Mwenyekiti Kamati ya Nidhamu, (kushoto) akiwa na Kassim Dau, mjumbe wa kamati hiyo wakati wakitangaza matokeo ya mwisho ya kamati yao jijini Dar es Salaam, leo.
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League).

Akisoma hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa vilabu na wenyeviti wa vya vyama vya mpira wa miguu vya mikoa jana, Wakili Msemwa amesema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi.

Klabu ya Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zimekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao.

Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C.

Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola na kamisaa wa mchezo huo Moshi Juma baada ya kukutwa na hatia ya upagaji matokeo.

Aidha kamati pia imemkuta na hatia kocha msaidizi wa klabu ya Geita Gold, Choke Abeid na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu. Magolikipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa na Dennis Richard wa Geita Gold wamefungiwa miaka 10 kutojihusisha na mpira wa miguu sambamba na kulipa faini ya shilingi milioni kumi (10,000,000) kila mmoja.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge, Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold, Cosntantine Moladi na Katibu wa klabu ya JKT Kanembwa Basil Matei wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu baada ya kutokutwa na hatia katika shauri hilo.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Fateh Remtullah, Mwenyekiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian wamefungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde wamefungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.

Katibu wa klabu ya Polisi Tabora, Alex Kataya, Katibu wa klabu ya JKT Oljoro, Hussein Nalinja, mtunza vifaa wa klabu ya Polisi Tabora, Boniface Komba, na Meneja wa timu ya  Polisi Tabora, Mrisho Seleman, wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu ya baada ya kutokutwa na hatia.


Kutokana na maamuzi hayo ya Kamati ya Nidhamu ya TFF, Kamati husika zitakaa kupitia Kanuni na kutangaza timu itakayopanda Ligi Kuu (VPL) msimu ujao na timu zitakazopanda Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes) msimu ujao.

IMETOLEWA NA MSEMAJI WA TFF, BARAKA KIZUGUTO

 

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKO NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
New Picture
TAARIFA KWA UMMA
Mnamo tarehe 01.04.2016 ilisambazwa taarifa ya uongo kwenye mitandao ya Kijamii ambayo kwa kiasi kikubwa ilipotosha Umma wa Watanzania kwamba kuna Kikao cha Baraza la Madiwani kilichokua kifanyike Tarehe 01.04.2016 kimevunjika na kuahirishwa hadi wiki ijayo kufuatia Waheshimiwa Madiwani kutoa hoja ya kutojadiliwa kwa Kabrasha mpaka hapo hoja mbili za nyuma zitakapojibiwa.
Tungependa wananchi waelewe kwamba taarifa hiyo si sahihi na inapotosha umma. Halmashauri ya Jiji la Arusha kama ilivyo Mamlaka zingine za Serikali za Mitaa Nchini inaendeshwa  kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa na Taratibu za uendeshaji wa vikao vya Halmashauri. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Halmashauti ya Jiji la Arusha kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilifanyika Feb 10, 2016 na kitaketi tena baada ya miezi mitatu.
Hii ina maana kwamba hakuna Kikao chochote kilichokua kifanyike Tarehe 01.04.2016 na wala hoja zilizotajwa kwenye taarifa hiyo si za kweli. Vikao vyote vya Baraza la Madiwani hutangazwa na Mkurugenzi wa Jiji kupitia vyombo vya Habari na viko wazi kwa Umma na mwananchi yoyote anaruhusiwa kuhudhuria.
Inawezeakana mtoa taarifa hizo pengine alikusudia kutumia tarehe 01 April kuwa siku ya wajinga lakini hakupaswa kutoa uongo kwa Umma katika maswala ambayo upotoshaji wake utaathiri jamii.
Napenda kuwaarifu watanzania wote kuipuuzia habari hiyo  kwani haina ukweli wowote.
IMETOLEWA NA:
AFISA HABARI
Kny: MKURUGENZI WA JIJI
ARUSHA
02.04.2016

WADAU, TAASISI NA MASHIRIKA WATAKIWA KUTOKUPUNGUZA KASI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA USAFI WA MAZINGIRA.

M1Viongozi wa DAWASA wakishiriki katika zoezi  la usafi.
Kutoka kushoto  ni Mary Ntukula, Mkurugenzi wa utawala na kulia ni Eng
 Romanus  Mwang’ingo Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi.  Katikati ni Neli
Msuya  Meneja mahusiano  ya jamii.M2Baaadhi ya watumishi wa DAWASA wakiendelea na zoezi la
usafi katika Hospitali ya Mwananyamala.M3Watumishi wa DAWASA na DAWASCO wakijiandaa kuingia kwenye
wodi za wagonjwa kugawa misaada ya vitu mbalimbali.M4
M5Watumishi wa DAWASA na DAWASCO wakigawa msaada wa vitu mbalimbali kwenye wodi za wagonjwa.M6
Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye pia ni Daktari
wa watoto, Delila Moshi akizungumza mara baada ya zoezi la usafi wa
mazingira na ugawaji  wa misaada katika hospitali hiyo uliofanywana
watumishi wa DAWASA na DAWASCO.
Picha na Aron MSigwa- MAELEZO.
…………………………………………………………………………..
Na.Aron Msigwa-MAELEZO.
Wito umetolewa kwa jamii, Taasisi na wadau mbalimbali kutopunguza kasi
katika kutekeleza kwa vitendo agizo la kufanya usafi wa mazingira,
kupanda miti na kulinda vyanzo vya maji alilolitoa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Desemba  9 mwaka jana.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam ( DAWASA) Bi.Mary
Ntikula kufuatia  watumishi wa Mamlaka hiyo na wale wa Shirika la Maji
Safi  na Maji Taka Dar esalaam (DAWASCO) kufanya Usafi na kukabidhi
msaada wa vitu mbalimbali hospitalini hapo amesema kuwa wao kama
DAWASA wamejiwekea utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo
yanayowazunguka kila mwisho wa mwezi kuunga mkono agizo la Mhe.Rais la
kufanya usafi kila jumamosi mwisho ya kila mwezi.
Amesema katika kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo utaratibu wa
kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka yakiwemo ya Hospitali
ya Mwananyamala na maeneo mbalimbali ikiwemo vyanzo vya maji pamoja
na shughuli za upandaji wa miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira.
Ameeleza kuwa Jumamosi ya kwanza ya mwezi huu wao kama DAWASA wameona
ni vyema wakaitumia kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali ya
Mwanayamala kwa kutambua mchango wa hospitali hiyo katika kuhudumia
afya za wagonjwa wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar
essalaam.
Ameongeza kuwa wao kama wafanyakazi wa DAWASA wameungana na wenzao wa
DAWASCO kufagia, kufyeka, kusafisha mifereji na kuondoa maji taka
katika hospitali hiyo pamoja na kutoa zawadi zinazoendana na usafi
zikiwemo maji, mafuta, sabuni za kuogea na kufulia pamoja na mafuta ya
kujipaka watoto wadodo na vitu mbalimbali kwa matumizi ya wagonjwa ili
kuonyesha upendo wao.
” Leo tumekuja hospitali ya Mwanayamala kufanya usafi na kutoa zawadi,
tumezunguka mazingira yote, tumefagia, tumefyeka, tumezoa uchafu na
pia kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa zinazohusiana na usafi na
nyingine tumewapatia viongozi wa hospitali ili waendelee kudumisha
usafi katika hospitali hii” Amesisitiza na kuongeza kwamba wao kama
DAWASA wataendelea kusaidia hospitali hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa DAWASCO Mhandisi Shabani
Mkwanywe amesema wao kama DAWASCO wameitikia wito wa Mhe.Rais kwa wa
kufanya usafi kila jumamosi ya kwanza ya kila mwezi kwa kugawanyika
katika maeneo mbalimbali kufanya usafi ikiwemo hospitali ya Muhimbili.
Amesema wao wanafanya kazi na jamii na wataendelea kuwajibika kwa
jamii kwa kile wanachokipata na kutoa wito kwa Taasisi na mashirika
mengine kuitumia siku hii kufanya usafi ili kuepuka magonjwa ya
milipuko.
Aidha, amesema DAWASCO katika kutekeleza majukumu yao wataendelea
kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kuondoa
changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa mkoa wa Dar es salaam na
wakazi wa Kibaha na Pwani mkoani Pwani ya uhaba wa maji kufuatia
uzalishaji wa maji ya kutosha uliopo sasa.
Naye Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye pia ni Daktari wa
watoto, Delila Moshi akizungumza mara baada ya zoezi la usafi wa
mazingira na ugawaji  wa misaada katika hospitali hiyo amewashukuru
watumishi wa DAWASA na DAWASCO kwa kujitoa na kufanya usafi.
Ameeleza kuwa hospitali hiyo licha ya kupata huduma ya uhakika ya maji
safi bado inakabiliwa na changamoto ya uondoaji wa majitaka kwenye
mashimo yaliyopo hospitalini hapo kutokana na mfumo wa uliopo
kutounganishwa kwenye mfumo mkuu unaopeleka maji taka baharini  jammbo
linaloifanya hospitali hiyo kujikuta ikitumia gharama kubwa kuondoa
maji hayo.
” Maji taka tunayozalisha kwa siku ni mengi sana, tunawashukuru DAWASA
na DAWASCO kujitolea kunyonya maji taka yote katika mashimo sasa
tutakaa miezi 6, ninyi wenyewe mtakua mashahidi gharama ya uondoaji wa
maji haya ni kubwa tumekuwa na kero ya vyoo kufurika na wakati
mwingine kuziba”
Aidha, amesema kuwa hospitali ianaendelea na mradi wa jengo la ghrofa
5 kwa lengo la kupunguza msongamano wa wagonjwa walioko kwenye wodi 11
ambazo zote zimejaa wagonjwa huku akibainisha kwamba hospitali hiyo
ina hudumia zaidi ya kniniki 11 pia wagonjwa 1500 hadi 2000 kwa siku.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuboresha huduma za afya hospitalini hapo kama
walivyofanya DAWASA na DAWASCO.
Nao baadhi ya wagonjwa wa hospitali hiyo waliopata fursa ya kuzumza
mara baada ya kukabidhiwa misaada hiyo akiwemo Bi.Stella Mkufya
anayeuguza mwanae katika wodi ya watoto hospitalini hapo ameishukuru
DAWASA na DAWASCO kwa misaada waliyoitoa.
Amesema kuwa mbali na kupokea misaada ya vitu anafurahishwa na ubora
wa huduma zinazotolewa kutoka kwa madaktari wa hospitali hiyo na
kuiomba Serikali iendelee kuongeza majengo na vitanda vya wagonjwa
katika hospitali hiyo.
” Nawashukuru DAWASA na DAWASCO kwa msaada waliotupatia pia
nawashukuru madakatari wa hospitali hii kwa huduma nzuri
wanayotupatia, kwa kweli huduma ya hapa ni nzuri sana naiomba Serikali
ituongezee vitanda na magodoro” Amesema.

NNAUYE ASHIRIKI MECHI KATI YA MBEYA CITY NA COASTAL UNION

N1Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanjaa (kushoto) alipowasili katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kuangalia mchezo kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makalla.N2Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union ya Tanga wakifanya mazoezi kabla ya kuanza mechi yao na Mbeya City jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.N3Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union na Mbeya City wakisakata kabumbu jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.N4Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifuatilia kwa makini mchezo wa mpira wa miguu kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jijini hapo. Kushoto kwa Mhe.  Nnauye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makalla na wakwanza kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndg. Halhaji Kundya.N5Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia ushindi wa timu yao ya Mbeya City baada ya kuichapa timu ya Coastal Union ya Tanga mabao manne kwa sifuri jana katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni