VARDY, APIGA MBILI LEICESTER, SUNDERLAND YATOKA HOI 2-0, HARUFU YA UBINGWA YANUKIA,,,
Leicester imeitungua Sunderland kwa mabao 2-0, yote mawili yakiwa yamefungwa na mshambuliaji wake hatari Jamie Vardy.
Vardy
amefikisha mabao 21 akiwa anakimbilia ufungaji bora, huku Leicester
iliyobakiza mechi tano tu za Ligi Kuu England ikiwa imeanza kusikia
harufu ya ubingwa.
Ushindi
huo unaifanya ifikishe pointi 72, nafasi ya pili Tottenham wakiwa na
pointi 62 na Arsenal katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 59.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni