NA RAYMOND URIO, Dar
Mshauri
wa benchi la ufundi la Taifa Stars ambaye pia ni Kocha wa JKT Ruvu,
Abdallah Kibadeni, ametangaza kuwa amepanga kustaafu kufundisha soka
hivi karibuni.
Kocha Kibadeni
ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa ndani ya Simba, Majimaji pamoja
na Taifa Stars, amesema kuwa kwa sasa hataki presha ya timu, hivyo anataka
apumzike.
Kibadeni amesema kama mchango ametoa wa kutosha katika timu mbalimbali hivyo sasa ni muda wake wa kupumzika.
“imefika kipindi na wakati wa kutulia na kuacha akili kutulia, unajua hizi timu zina presha
sana na ukiangalia umri umeenda nimeona ni bora nipumzike.
“Hivi
karibuni nitatangaza kuachana na ukocha wa hizi timu za wakubwa
nitadili na kituo changu tu cha Kibadeni Sports Academy (Kisa), najua
huku hawa watoto pamoja na timu kuwa siyo ya ushindani sitapata presha,”
alisema Kibadeni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni