MTAMBO WA RUVU JUU KUZIMWA KWA SAA 14.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Shirika la Maji Safi na Maji taka 
Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza kuzima mtambo wa kuzalisha Maji wa 
Ruvu Juu kwa wakazi wa Dar es salaam na Mji wa Kibaha Pwani kwa saa 14 
kesho Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano usiku.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa 
kwa vyombo vya Habari  na ofisi ya mahusiano ya shirika hilo leo  jijini
 Dar es Salaam inaeleza kuwa sababu kuu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni 
kuruhusu usafishaji wa bomba jipya na kufanya majaribio ya sehemu ya 
mtambo mpya wa Maji wa Ruvu juu.
Pia zoezi hili linahashiria hatua 
za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo
 la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo
 huo.
Maeneo ambayo yatakosa maji ni 
Mlandizi Mjini , Ruvu darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, 
Janga, Mbagala, Visiga, Lulinzi, Kibamba, Kibamba njia panda, Shule 
kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba hospital, Kwa mkinga, Luguruni 
,Maili 35, Zogowale, Misugusu,Tanita, Kibondeni, Kwa mathias, Nyumbu, 
Msangani, Kwa mbonde, Picha ya Ndege, Sofu na Gogoni.
Pia zoezi hili linahashiria hatua 
za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo
 la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo
 huo.
Aidha Shirika linatoa ushauri kwa  wananchi  kuhifadhi maji na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni