Ijumaa, 9 Septemba 2016

NDIKILO:WALIOJENGA NDANI YA MITA 60 MAIL MOJA ,WAFUNGE VIRAGO



unnamed

Mwenyekiti wa bodi  ya barabara mkoani Pwani ,ambae pia ni mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo,akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara mkoa ,kulia ni katibu tawala mkoani humo Zuberi Samataba na kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoani hapo Mwinshehe Mlao.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
BODI ya barabara mkoani Pwani ,imewatahadhalisha wafanyabiashara na wananchi wa Mailmoja,Mji wa Kibaha,ambao wamejenga kwenye eneo la hifadhi ya barabara ,kuanza kubomoa kwa hiari ,kabla ya novemba 23.
Imesema  wakala wa barabara (TANROADS )ilishawaandikia barua watu waliojenga kwenye eneo la hifadhi ya barabara umbali wa mita 60 kwa kila upande wa barabara kuu ya Morogoro kuanzia Kiluvya -Tamco kwa kipindi kirefu sasa.
Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara mkoani Pwani,mwenyekiti wa bodi hiyo mkoani humo,mhandisi Evarist Ndikilo,alisema wakala huo utaanza kubomoa eneo la mita 60 badala ya 120 zilizoelezwa awali.
Alieleza kuwa ni wakati wa jamii kukubali mabadiliko hayo ambayo yapo ndani ya sheria ili mji wa Kibaha uweze kuwa katika mpangilio mzuri.
Mhandisi Ndikilo alisema kipindi cha nyuma wananchi walipinga kufanyika kwa bomoabomoa lakini walishindwa kesi walizofungua hivyo kwasasa ni vyema wakapisha maeneo hayo bila shuruti.
“Tanroads ikifika novemba 23 mwaka huu itavunja eneo la Mailmoja na haiwezi kurudi nyuma”
“Lengo letu ni halmashauri ya Mji kuwa manispaa hivyo moja ya vigezo ni kupanga Mji huu ,wananchi watuelewe na wote tunahitaji kupanga Mji wetu alifafanua mwenyekiti huyo .
Alieleza kuwa kutokana na sintofahamu ya hifadhi ya mita 120 ama mita 60 kila upande hadi hapo wizara ya ujenzi itakapotoa ufafanuzi hivyo wakala huo utaanza kubomoa upana wa mita 60.
Mwenyekiti huyo ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Ndikilo,alisema wananchi waanze kufunga virago na hakuna mjadala kuhusiana na hilo.
Nae mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo alisema soko la sasa litahamia eneo la Sagulasagula na fedha zipo na tangazo la kumpata mkandarasi limeshatoka.
Alisema soko la Sagulasagula linatarajia kukamilika mwezi wa 12 mwaka huu.
Hata hivyo ,Jennifer alielezea kuwa wafanyabiashara wanaofanya biashara kwenye eneo la Mailmoja wawasiliane na halmashauri kupata maeneo pembezoni mwa soko la Sagulasagula kwa ajili ya kujenga mabanda yao.
Jennifer aliwaomba wafanyabiashara hao kuanza kuwasiliana na halmashauri  ili  waanze kuchukua maeneo na kuajenga mapema.
Pia alisema  maeneo ya Mailmoja yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara yatabomolewa lakini stend itaendelea kufanya kazi hadi hapo itakapojengwa stend mpya .
Jennifer alisema endapo zoezi la  bomoa bomoa litafanyika itawasaidia halmashauri kupanga Mji na kuwa na kujenga mabanda ya kupumzikia abiria eneo la  stend  ya sasa.
Meneja wa Tanroads mkoani Pwani, Tumaini Sarakikya alisema awali zoezi hilo lilikuwa lifanyike mwezi agost lakini muda uliongezwa hadi mwezi novemba na kudai wapo watu wengine walishawekewa alama ya X tangu mwaka 2004 .
Alisema katika kipindi hicho chote zoezi hilo halikufanyika ila kwasasa ndio linatarajiwa kutekelezwa na hawawezi kurudi nyuma.
Sarakikya alisema wananchi walikwenda mahakamani ambapo walishindwa kesi.
Anasema kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 1932 na kufanyiwa marekebisho 1958 kifunga na 52 na marekebisho ya sheria ya barabara na 13 ya mwaka 2007 .
Taratibu za sheria za usimamizi wa barabara kifunga na 30 (b) eneo la hifadhi ya barabara,mita 120 sawa na futi 400 kwenda kila upande kutoka katikati ya barabara ni marufuku kufanya maendelezo yoyote katika eneo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni