KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA VIZUIZI VYA BARABARANI (MIZANI)
Katibu
 Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua 
akiweka sahihi katika kitabu cha wageni wakati wa ziara yake katika 
Vizuizi vya barabarani (Mizani) na Mipakani kwa lengo la kufanya 
Tathimini ya Utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya biashara
 na uwekezaji nchini Septemba 15, 2016.
Msimamizi
 wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato TRA kilichopo Mkoani Pwani Bw. David 
Kisanga akitoa maelezo juu ya utendaji wa ofisi zao kwa Katibu Mkuu 
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati 
alipotembelea ofisi hizo Mkoa wa Pwani. 
Katibu
 Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua 
akimsikiliza Msimamizi wa Kizuizi cha Vigwaza Mkoani Pwani Bw. Titus 
Michael wakati wa ziara yake kujionea hali halisi ya vituo hivyo 
kwaajili ya Maboresho ya mazingira ya biashara na Uwekezaji nchini. 
Baadhi ya magari yakipima uzito wa mizigo katika Mizani ya Vigwaza mkoa wa Pwani, Septemba 15, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni