RC ARUSHA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI
| Mkuu
 wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na 
Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) alipomtembelea ofisini kwake | 
|  | 
| Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo. | 
|  | 
| Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya mazungumzo yao. | 
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea  na  ziara yake ya kujitambulisha kwa
viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Mchungaji Solomon Masangwa , Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.

Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira
ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph  Magufuli
 kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani  halmashauri 
zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya  mikopo 
yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali  zitakazowawezesha
 kufanya  shughuli za uzalishaji mali.
Amewataka  wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari  kupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa  elimu
 kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe 
inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala 
kisiasa.
Askofu
 Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na
 kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye 
Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya 
uvunjifu wa amani. 
Aidha alishauri  kutokana
 na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya 
Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha 
uliopo Kisongo  ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya
kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh.
 Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha
 mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili  watoe mawazo yao 
katika kuiboresha na  kuifanya itekelezeke   kwa wepesi zaidi.
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni