Jumamosi, 17 Septemba 2016

Msingi wa Usomaji bora ni mtoto kujua kusoma kwa wakati.

Text Box: World Change Starts with Educated Children®


Msingi wa Usomaji bora ni mtoto kujua kusoma kwa wakati.

Tanzania kama nchi nyingi zinazoendelea bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na wananchi wasiojua kusoma na kuandika ndani ya mfumo wa elimu na nje ya mfumo wa elimu, na hii ndio sababu, RoomtoRead imeamua kuandaa mjadala huu wa wadau wa usomoji ili tutafakari na kuweka mikakati ya kuwa na taifa lisilokuwa na wasiojua kusoma – Peter Mwakabwale: Mkurugenzi mkaazi wa Room to Read Tanzania .

Takwimu zinaonyesha asilimia 22 Ya watanzania wote hawajui kusoma na kuandika.  Takwimu hizi haziishii kuwa takwimu kwa maana ya namba tu, bali hawa ni watanzania wenzetu, wapiga kura, wateja wa huduma zetu, wazazi wetu na vijana wetu ambao wataongoza taifa hili kwa miaka kadhaa ijayo.  Watanzania inabidi tujiulize ni nini kimetokea? Miaka ya 70 na 80 watanzania wengi walikuwa wanajua kusoma na kuandika, kinyume na sasa ambapo teknolojia imekuwa Zaidi, shule ziko nyingi Zaidi nk.


Kutojua kusoma na kuandika hakukwamishi tu mapambano yetu dhidi umaskini bali kuna athari za moja kwa moja katika biashara, kwa mujibu wa bwana Noel Mazoya- Meneja wa Masoko Vodacom, “Taasis kama Vodacom, inatumia muda na pesa nyingi sana kuwafikia wateja wao ana kwa ana kwa sababu tu baadhi ya wateja wao, hasa wa vijijini hawajui kusoma na kuandika hivyo kushindwa kuwafikia kwa njia wa ujumbe mfupi au kidigitali”.

Vyombo vya habari na wasanii wananafasi kubwa katika kuongeza au kuhakikisha janga hili la ujinga litatokomezwa. Hapa nchini Tanzania, baadhi ya vyombo vya habari vinachangia kukuza tatizo la kutojua kusoma “Msingi wa vyombo vya habari ni kufundisha, kufurahisha na kuhabarisha, ila kwa sasa, kuna vyombo vya habari pendwa, vinavyotoa habari nyepesi hata kama hazina mwelekeo wa kuikuza jamii hiyo,”. Victor Eliah – Television ya Taifa

Sanaa ndio kitu cha kwanza kinachotumika kumfundisha binadamu, kwa mfano, watoto wa shule za awali wanajifunza kwa michoro na nyimbo. Tunahitaji wasanii wanajua umuhimu wa kusoma na elimu ili waweze kutunga Sanaa yenye kuijenga jamii. Wananchi wawekuwa chanzo cha tatizo kwa kutothamini kazi za Sanaa zenye kuelimisha badala yake, huthamini na kazi za Sanaa zenye kuburudisha tu - Vitalis Maembe (Msaanii Mkongwe) 

Jitihada za wadau wa elimu katika kuhakikisha kila mtoto anajua kusoma kwa wakati, zinahitaji mazingira mazuri ya kisera.  “Kuwepo kwa sera mpya ya elimu bure ni jitahada zinazotakiwa kupongezwa” ingiwa takwimu za taasis mbalimbali zinaonyesha kiwango cha elimu yetu kinashuka, mfano 16% ya wanafunzi wa darasa la saba hawawezi kusoma habari ya darasa la pili. John Kallaghe, Mkurugenzi wa Hakielimu Tanzania

Mapendekezo ya Wadau:
1.     Ni lazima tujikite katika kuwekeza katika watoto walioko nje ya shule, watoto million 2 wako nje ya shule na hawajui kusoma na kuandika.
2.     Ubora wa elimu hauwezi kuja bila uwekezaji timilivu. Serikali inabidi iongeze fungu la bajeti ya elimu hasa bajeti ya elimu elimu ya msingi.
3.     Walimu ndio chachu ya mabadiliko katika kuboresha ubora wa elimu yetu,Kubadilika kwa mitaala kuendane moja kwa moja kuwekeza kwenye ubora wa walimu
4.      

Kwa namna ya pekee serikali inathamini sana mchango wa taasis sizizo wa kiserikali katika kuboresha  ubora wa elimu nchini Tanzania – Waziri Simbachawene.






Rejea
Room to Read, ni shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linalolenga kubadilisha maisha ya watoto katika nchi zinazoendelea kupitia uboreshaji wa mazingira ya kusoma na kujisomea pamoja na elimu bora kwa watoto wa jinsia zote. Shirika lilianzishwa mwaka 2000 kwa filosofia ya kuwa “Mabadiliko ya Dunia Yanaanza na Watoto Walioelimika”. Room to Read wanaiona dunia yenye mazingira yanayomuwezesha kila mtoto kupata elimu bora itakayomuwezesha kukua na kuweza kutoa mchango katika jamii yake na hata kwa dunia nzima.

Mfumo wa miradi ya Room to Read umejengwa katika Nyanja kuu mbili:
·         Wakati wa awali wa Elimu ya msingi kwa ajili ya kukuza usomaji.
Tunafanya kazi na jamii pamoja na serikali kuimarisha stadi za usomaji na tabia ya kujisomea kwa watoto wa shule za msingi.
·         Wakati wa elimu ya sekondari; kwa elimu  ya wasichana:
Tunahakikisha msichana anaweza kumaliza elimu ya sekondari akiwa na stadi za maisha zinazomuwezesha kuyakabiri mazingira anayoishi.

Room to Read inaendesha miradi yake katika nchi 10 duniani ikiwemo, Bangladesh, Cambodia, India, Laos, Nepal, Afrika ya Kusini, Sri Lanka, Tanzania, Vietnam na Zambia, na imelenga kuwafikia watoto milioni 20 ifikapo mwaka 2020.
Nchini Tanzania, Room to Read imeanza kufanya kazi mwaka 2011, kwa kuanzia Mkoa wa Morogoro, wilaya ya Mvomero, na baadae kuongeza miradi yake katika mkoa wa Pwani, katika halmashauri za wilaya ya Bagamoyo, Chalinze na Kibaha.
Miradi inayotekelezwa nchini Tanzania ipo katika Nyanja kuu tatu:

1.      Ujenzi na ukarabati miundombinu shuleni:
·         Ujenzi wa Maktaba na
·         Ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi

2.      Stadi za Usomaji:
·         Uandishi wa vitabu vya haditihi za watoto, vitabu vya walimu vya kufundishia na vya wanafunzi vya kujifunzia.
·         Kuwafunza walimu wa darasa la kwanza na la pili mbinu za ufundishaji
·         Kuwafundisha na kuwaandaa walimu wakutubi

3.      Elimu ya Stadi za Maisha kwa Wasichana:
·         Kutoa elimu za stadi za maisha kwa wasichana
·         Kuwasaidia wasichana waliochaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari wanaotoka katika familia zenye uwezo duni.

Mafanikio:

Hadi leo, Room to Read imeweza kushirikiana na shule za msingi 98 za serikali katika halmashauri nne za  Mvomero, Bagamoyo, Chalinze and Kibaha vijijini na kuwa na mafanikio yafuatayo:

·         Kujenga vyumba 113 vya madarasa
·         Kujenga Maktaba 98
·         Kukarabati vyumba vya madarasa 34
·         Kuandika na Kuchapisha vitabu 89,000 vya Hadithi za watoto kwa Kiswahili
·         Kununua na Kugawa vitabu 112,000 vya Hadithi za watoto za kiswahili    
·         Kufundisha walimu 35 wa darasa la kwanza
·         Kufundisha walimu 35 wa darasa la pili
·         Kufundisha wakuu wa shule za msingi zipatazo 77
·         Kufudisha waalimu wa taaluma 26
·         Kufundisha waalimu wakutubi wa shule za msingi zipatazo 77 katika Nyanja ya utawala na uendeshaji shughuli za maktaba
·         Kufundisha Maafisa elimu wanne wa halmashauri nne za wilaya 
·         Kufundisha wakaguzi elimu wanne wa halmashauri nne za wilaya
·         Kufundisha Waratibu elimu kata 19
·         Shule 9 za sekondari zinapata msaada wa elimu kwa wasichana
·         Shule 9 za sekondari zinapata ruzuku kwa ajili ya masomo ya ziada kwa wasichana
·         Wasichana 1906 wa sekondari wamenufaika na wanendelea kunufaika na mradi

·         Watoto wapatao  48000 wa shule ya msingi wanafaidika na mradi





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni