TUME YA MIPANGO YAKAMILISHA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA UMMA MIKOA YA SINGIDA, MANYARA NA DODOMA
Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (katikati) akitoa hotuba ya kufunga mafunzo ya Usimamizi
 na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma kanda ya 
kati iliyojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara katika ukumbi wa 
VETA mjini Dodoma. Kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma 
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu 
Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla,Tume ya Mipango, dkt. Lorah Madete.
Washiriki wanaounda kundi la nne wakijadili maswali juu ya utayarishaji na uchaguzi wa Miradi ya uwekezaji.
Washiriki kundi la kwanza wakijadili maswali waliyopewa na wakufunzi kabla ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo Septemba 16, 2016.
Washiriki kundi la pili wakifanya maswali  waliyopewa na wakufunzi mara baada ya kuhitimisha somo.
Na Adili Mhina, Dodoma.
Tume 
ya Mipango imehitimisha mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi 
ya Uwekezaji katika sekta ya Umma yaliyowahusisha maofisa mipango wa 
Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Singida, Manyara na
 Dodoma yaliyofanyika tarehe 12-16 Septemba, 2016 katika ukumbi wa VETA 
mjini Dodoma.
Akifunga
 mafunzo hayo Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi 
Florence Mwanri aliwasihi washiriki kutumia ujuzi waliyoupata katika 
kuandaa, kutekeleza miradi ya Umma kwa njia za kisasa ili kuongeza 
ufanisi wa miradi na kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Alisema
 kuwa Tume ya Mipango imefanikiwa kutekeleza wajibu wake wa kuwajengea 
uwezo maafisa hao katika hatua zote muhimu zinazopaswa kuzingatiwa 
katika kufanya maandalizi, kutekeleza, kusimamia, kufuatilia na kufanya 
tahmini ya miradi ya maendeleo.
“Ni 
matumaini yangu kuwa hizi siku tano hazijapotea, mmepata elimu ya 
kutosha kutoka kwa wataalamu wetu katika masuala yote muhimu yanayohusu 
miradi ya Umma. Jukumu mlilonalo kwa sasa ni kuhakikisha mnatumia mbinu 
mlizofundishwa katika kutekeleza miradi ya serikali kwa usahihi ili 
tufikie malengo ya  mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano,” 
Alisema.
Nao 
washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuwa wamepata elimu muhimu ambayo 
itarahisisha utendaji katika kusimamia miradi na kutoa ushauri wa 
kitaalamu katika ngazi mbalimbali za maamuzi.
Walieleza
 kuwa mafunzo hayo yamewasisitiza kutumia vigezo muhimu wakati wa 
kufanya uchambuzi wa kiuchumi na kifedha ili kufikia uamuzi wa kutambua 
miradi ipi ina manufaa na inaweza kupata mikopo katika soko la mitaji.
“vigezo
 kama mzunguko wa mradi (project cycle) ikiwa ni pamoja na andiko la 
awali (concept note), mchanganuo wa faida na hasara (cost-benefit 
analysis) vigezo vya kuchanganua mradi kama vile uwezo wa uzalishaji 
(internal rate of return)  na thamani halisi ya uwekezaji (Net 
Present Value) vimetolewa ufafanuzi mzuri na vimeeleweka na tumevielewa”
 Alisema mmoja wa wakufunzi aliyejulikana kwa jina la Jemsi.
Tume 
ya mipango inaendelea na zoezi lake la kutoa mafunzo kwa walengwa wakuu 
ambao ni wataalam wa Sera na Mipango ambapo kuanzia Septemba 19 
wataalamu wa mafunzo hayo watakuwa Mkoani mbeya kwa ajili ya zoezi hilo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni