Sophia Mjema Akabidhi Msaada Muhimbili Leo
Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Sophia Mjema akipokea msaada wa kitanda cha wagonjwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoka Kikundi cha Itambue Thamani
Yako cha jijini Dar es Salaam LEO.
Mkuu wa Wilaya ya
Ilala jijini Dar es Salaam, Sophia Mjema akisalimiana na kina mama wa
kikundi hicho leo baada ya kupokea msaada wa kitanda hicho.
Mkuu huyo akitembelea chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) leo katika hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Magreth Makwesa akizungumza na vyombo vya habari leo kabla ya kukabidhi msaada.
Kinamama wa kikundi hicho wakiwa katika picha ya pamoja leo katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Sophia Mjema (aliyefunga kitambaa cha bluu) akiwa katika picha ya
pamoja na kinamama wa kikundi cha Itambue Thamani Yako leo.
……………………………………………………………………………….
Na John Stephen, MNH
Dar es Salaam, Tanzania. Mkuu wa
Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Sophia Mjema amewataka watu
wajitokeze katika kusaidia sekta ya afya nchini.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema
hayo Leo wakati akipokea msaada wa kitanda kutoka katika Kikundi cha
kinamama cha Itambue Thamani Yako cha jijini Dar es Salaam.
“Watu wajitokeze kusaidia vifaa
tiba kama walivyofanya wenzetu wa kikundi cha Itambue Thamani Yako.
Nawapongeza kina mama kwa jitihada zenu,” amesema mkuu huyo.
Baada ya kupokea msaada huo,
Mjema ametembelea chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu
(ICU) na kuona jinsi huduma zinavyotolewa.
Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho, Magreth Makwesa amesema kwamba kitanda hicho kina thamani ya Sh3.5 milioni.
Amesema malengo ya kikundi hicho
ni kina wanachama 40 na kwamba malengo yake ni kusaidiana katika shida
na raha, kuinuana kiuchumi na kuisadia jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni