Ijumaa, 9 Septemba 2016

MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS WAPATA AJALI KIJIJI CHA NAGURUWE MTWARA UKIELEKEA TANDAHIMBA


aj5

Askari wa vyombo vya ulinzi na usalama wakisaidia kuokoa majeruhi wa ajali hiyo.
…………………………………………………………………………
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Mtwara
Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa Channel Ten, Startv na Clouds Tv liliacha njia na almanusura lipinduke.
Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.aj1
Majeruhi wakisaidiwa baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
aj2 aj3
Askari wa vyombo vya ulinzi na usalama wakisaidia kuokoa majeruhi wa ajali hiyo
aj4 
Majeruhi wakipata huduma ya kwanza baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni