PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DKT. JULIANA PALLANGYO JIJINI DAR ES SALAAM
Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya Idara ya Nishati katika kikao hicho.
Profesa Mark Mwandosya akisisitiza jambo katika kikao hicho
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Profesa Mark Mwandosya (hayupo pichani)
Kutoka kulia, Profesa Mark Mwandosya, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile na mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi kutoka katika kampuni ya Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakiwa katika picha ya pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni