Wafanyakazi wa TBL wasafisha mazingira Ilala Mchikichini
Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha
Ilala (TBL Group) wakifanya usafi kwenye mfereji wakupitisha maji
machafu uliopo katika Mtaa wa Mission Kota ya Mchikichini Ilala jijini
Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Kiwanda cha
bia cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Nkondola (kushoto)
akibadilishana mikakati ya usafi na Diwani wa kata ya Mchikichini
Joseph Ngowa ( kulia) . Katikati ni Afisa usalama na Afya wa TBL Group,
Khery Gunzarethy.
Afisa Mwandamizi wa kiwanda cha
TBL cha Ilala Charles Nkondola akishirikiana na wafanyakazi wenzake
kufanya usafi kwenye mtalo wa kupitisha maji machafu wa Mission uliopo
katika kata ya Mchikichini jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha
TBL Ilala jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na Afisa usalama na Afya wa
TBL Group, Khery Gunzarethy wakifanya usafi kwenye mtalo wa kupitisha
maji machafu uliopo katika kata ya Mchikichini .
Wafanyakazi wa Kiwanda cha bia cha
TBL Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Kata ya Mchikichini mara baada ya kumalizika kwa zoezi la
kufanya usafi wa mfereji wa Mission Kota .
……………………………………………………………..
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL
Group kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam jana walitumia sehemu ya
muda wao kwa kushiriki kwenye shughuli za jamii ambapo walisafisha
maeneo ya Ilala Mchikichini.
Zoezi hilo ni moja ya mkakati wa
kampuni wa kutunza mazingira kwa vitendo ambapo pia wafanyakazi wake
kutoka viwanda vyake vyote nchini mara kwa mara wamekuwa wakishiriki
katika shughuli za usafi mara kwa mara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni