Wafugaji wamwomba Rais Magufuli kuwanusuru ng’ombe wao
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji
Tanzania (CCWT), Maghembe Makoye akizungumza na waandishi wa habari
wakati akifafanua mambo mbalimbali kuhusu wafugaji walionyaganywa mifugo
yao na uongozi wa hifadhi ya Pori la akiba Katavi , Kushoto ni mfugaji
anayelalamikia kunyang’anywa mifugo yake Mayunga Gamasa na kulia ni
mfugaji Charles Mtokambali.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji
Tanzania (CCWT), Maghembe Makoyeakionyesha hukumu iliyotolewa na
mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga ili wafugaji hao warudishiwe mifugo yao
kushoto ni Mayunga Gamasa mfugaji na kulia ni mfugaji Charles
Mtokambali.
………………………………………………………………………………
NA MWANDISHI WETU
WAFUGAJI wa mkoa wa Katavi,
wamemwomba Rais John Magufuli kuwasaidia kurejeshewa mifugo yao 1,600
ambayo imeshikiliwa na watendaji wa hifadhi ya Katavi.
Wamesema mifugo hiyo aina ya
ng’ombe ilikamatwa Machi mwaka huu na kufunguliwa kesi lakini baada ya
kesi hiyo walishinda na kuamliwa kurejeshewa ng’ombe zao lakini mpaka
sasa amri hiyo haijatekelezwa.
Wakizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam wamesema, kutokana na unyanyasaji
wanaofanyiwa na watendaji hao wa hifadhi, Rais Magufuli ambaye ni
mtetezi wa wanyonge atupie jicho suala lao na kulimaliza.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji
Tanzania (CCWT), Maghembe Makoye alisema wafugaji waliochukuliwa mifugo
yao hivi sasa familia zao zinaishi maisha ya shida kwani hawana njia
mbadala wa kupata fedha na ufugaji ndiyo tegemeo lao.
“Tunamwomba Rais Magufuli aingilie
kati jambo hili ili Watanzania hawa wanyomge wapate haki yao.
Tunanyanyasika katika nchi yetu, huku chini kuna watu wanaendesha
serikali zao, hawajui juu kuna Magufuli, tunamwomba sana Rais alione
hili,” alisema Makoye
Alisema agizo la Rais la kuwataka
wakuu wote wa mikoa kubaini na kutenga maeneo kwa ajili wafugaji nchini
limeshindwa kuchukuliwa kwa uzito wake mpaka sasa hivyo umefika wakati
wa kulifanyia kazi.
Katibu huyo alisema katika
kufanikisha agizo hilo la Rais Magufuli kwa ufanisi, wameomba
kushirikishwa ili kumaliza migogoro iliyopo kati ya wafugaji na
wakulima.
Naye Mayunga Gamasa alisema kati
ya ng’ombe hizo 1600 yeye zake ni 552 ambazo kukamatwa kwake zimemfanya
kuwa masikini huku familia yake yenye watu zaidi ya 70 ikiishi kwa shida
kwani chanzo cha mapato ndiyo hicho kimeondoka.
“Mimi nina watoto 28, waijukuu 24,
wake wane jumla na wasaidizi kama watu 70, sasa ng’ombe hawa ndiyo
msaada kwangu, lakini uongozi wa hifadhi ya Katavi haitaki kutupatia
licha ya kushinda kesi, tunaomba Rais atusaidie” alisema Gamasa
Naye Charles Mtokambali mwenye
ng;ombe zaidi ya 700, alisema kunyimwa kwa ng’ombe hao kumebadili maisha
yake kwani kwa sasa familia yake haijui kesho yake, kutokana na
watendaji hao wa hifadhi huku akisema ana imani kubwa na Rais kwamba
atalishughulikia suala hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni