Ijumaa, 9 Septemba 2016

WAZAZI WALIOTELEKEZA WATOTO MTAANI KWA KUSHINDWA KUWAJIBIKA KUWALEA KUAWAJIBISHWA


arusha
Na Mahmoud Ahmad ARUSHA
SERIKALI wilaya ya Arusha, imewataka wazazi ambao wamewatelekeza watoto wao mitaani  kwa kushindwa kuwalea  kuhakikisha wanawajibika  kuwaondoa na kuwarejesha majumbani na kuwapatia malezi bora,badala ya kuwaacha waendelee kuishi kwenye mazingira magumu.
Hayo yalielezwa  na mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro, alipokuwa akifungua  mafunzo  ya utambulisho  wa mfumo  wa manegmenti  ya kesi za watoto  kwa wadau wa huduma  ya ulinzi na usalama  wa watoto katika jiji la Arusha na wilaya ya Karatu.
Daqarro, alisema katika jiji la Areusha kuna watoto waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi wapatao 18834,kutokana na wazazi  kutokutimiza wajibu  wa kuwalea ,hivyo umefika wakati wazazi lazima wahakikishe wanawaondoa watoto kwenye mazingira  hayo hatarishi vinginevyo serikali itawalazimisha.
”Serikali haitaki kuona watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na hatarishi  huku wazazi wao wapo “‘alisema Daqarro.
alisema haiwezekani wazazi kuwaacha watoto wakihangaika na kutaabika mitaani  na kukosa haki zao za msingi  zikiwemo elimu, afya,malazi ,lishe bora   na upendo, hivyo lazima wahakikishe  wanawarejesha majumbani watoto wao.
Aidha, aliupongeza mpango huo ambao umewezesha  jiji la Arusha, kuweza kusimamia  huduma mbalimbali  za watoto  kwa kuwa wangelikuwa kwenye hali mbaya  kutokana na mazingira waliyokuwa wakiishi.
Ameutaja mpango huo wa Pamoja Tuwalee umesaidia watoto kupata ulinzi ,usalama , afya na kuiwezeshja jamii kutoa mafunzona huduma kwa watoto waishio kwenye mazingira hatarishi.
Aliwataka mganga mkuu wa jiji la Arusha na Idara ya ustawi wa jamii, kuhakikisha  wanazingatia matumizi sahihgi ya mfumo huo ili kuepuka  kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha walengwa kwa kutambua wahitaji.
Awali, mkurugenzi wa shirika World Education ,Hindu Ally Mbogo, alisema  mpango huo wa Pamoja Tuwalee unafadhiliwa na shirika la misaada la Marekani, USAID, umesaidia kuokoa maisha ya watoto  waliopo kwenye mazingira hatarishi.
Alisema mpango huo kuwafikia watoto  na kuwapatia huduma mbalimbali  ikiwemo kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa taifa wa Pamoja Twaweza Program, Liliani Badi Manara, alisema  awamu ya kwanza ya mradi huo inakamilika Novemba 2016
Aidha awamu ya pili ya mradi huo wa miaka mitano unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID, itatekelezwa na shirika la Pact Tanzania

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni