UVCCM WATOA POLE TETEMEKO LA ARDHI
Majeneza ya miili ya watu
waliopoteza maisha jana kutokana na tetemeko la ardhi lililopokea mjini
Bukoba mkoani Kagera waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho na kuaga
miili ya marehemu hao leo kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambapo
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa ataongoza wananchi wa Bukoba kutoa
heshima za mwisho kwa miili ya marehemu hao.
…………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umetuma
salamu za pole wananchi wa mkoa wa Kagera kutokana na vifo vya zaidi ya
watu 11 vilivyosababisha na tetemeko la ardhi lililotokea juzi.Katika salamu hizo zilizotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVVCM, Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya umoja huo, alisema wamepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya vifo hivyo.
Alisema tetemeko hilo ni pigo kwa UVCCM na taifa kwa ujumla kwa kuwa limesababisha vifo vya watu ambao ni nguvu kazi ya taifa pia kusababisha hasara kutokana na uharibifu wa mali mbalimbali na makazi.
“UVCCM tumepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo kubwa na zito ambalo limesababisha maafa na hasara kwa taifa,”alisema.
Alisema umoja huo unawaombea marehemu wa tukio hilo wapate pumziko la milele peponi na kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurudi kwenye shughuli zao za kawaida.
“Katika kipindi hiki kigumu Jumuia yetu inaungana na Watanzania wengine kuzipa mkono wa pole familia zote zilizopoteza ndugu zao na pia tukiwafariji wote waliopata hasara ya kuharibikiwa nyumba zao na kupoteza mali,”alisema.
Alisema janga hilo ni limemgusa kila mtanzania mwerevu mwenye upendo na uzalendo hivyo linapaswa kuwaweka pamoja Watanzania wote ili kufarijiana na kukabiliana na magumu yaliyotokea.
Aidha, Shaka alisema wanatoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kutokana na vifo hivyo na kasara iliyopatikana.
Shaka aliwashukuru na kuwakupongeza viongozi wa umoja huo walioko mkoani humo wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Yahya Kateme, kwa ushirikiano walioendelea kuutoa baada ya kutokea kwa tukio huilo.
Huu si wakati wa siasa bali ni kipindi kigumu cha kukabili yale yote yaliotokea na kudhuru au kuharibu taaswira iliokuwepo awali ya ustawi wa maisha ya wenzetu ambao wamepatwa na janga hilo.
Kila kijana mzalendo ni vyema akaenda kuripoti kwa viongozi wa maeneo husika aidha wakuu wa wilaya au mkoa ili kupewa maelekezo na miongozo katika kila hatua ya kusaidiana kwa hali na mali wakati wote hadi hali itakaporejea kama kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni