UJENZI WA UKUTA WA OCEAN ROAD KUANZA HIVI KARIBUNI
Bw. Bernard Odhuno Msimamizi wa
Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na
Temeke (kwa niaba ya Ofisi ya Makamu wa Rais) akibadilishana Mkataba na
Bw. Sheikh Bawazir Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dezo Civil
Contractors iliyopewa kazi ya Ujenzi wa Ukuta wa (Ocean Road na
Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na
Temeke.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Eng. Ngosi Mwihava (wa kwanza kushoto) akishudia utiaji saini wa
Mkataba wa ujenzi wa Ukuta wa (Ocean Road na Kigamboni) na Ujenzi wa
Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke. Ujenzi huo
utafanywa na Kampuni ya Dezo Civil Contractors. Wengine katika picha ni
wawakilishi wa Kampuni ya Dezo na Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa
Rais.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni