PROF.MBARAWA AZINDUA KIVUKO CHA MV .TANGA NA GATI YA BANDARI YA PANGANI
Mbunge wa Jimbo la Pangani Mhe.
Jumaa Awesu akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo katika uzinduzi wa
Kivuko cha Mv. Tanga na Gati ya bandari ya Pangani uliofanyika Mkoani
Tanga.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) Eng.Karim Mattaka akisoma taarifa ya ujenzi wa
Gati ya bandari ya Pangani kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) katika uzinduzi wa
Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndg. Martin
Shigela akielezea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu katika
Mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa (hayupo pichani) katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga
na Gati hiyo uliofanyika Mkoani Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wananchi wa
Pangani katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Tanga na Gati hiyo uliofanyika
Mkoani Tanga.
Wananchi wa Pangani wakishangilia
ujio wa Kivuko kipya cha Mv. Tanga Wilayani hapo kinachotoa huduma ya
usafirishaji kati ya Pangani na Bweni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na watendaji wa Serikali na
Wizara wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Tanga
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pamgani Mhe. Zainabu Abdallah Issa .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na watendaji wa Serikali na
Wizara wakizindua Gati la Bandari ya Tanga.Ukamilifu wa Gati hiyo
utasaidia Meli mbalimbali kuweza kutia nanga wilayani Pangani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akisafiri na wakazi
katika Kivuko cha Mv.Tanga kutoka Pangani kwenda Bweni mara baada ya
uzinduzi. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi)
Eng. Joseph Nyamhanga.
…………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezindua kivuko kipya na cha kisasa
cha Mv. Tanga kinachotoa huduma ya usafirishaji kati ya Pangani na Bweni
na kuzindua Gati ya Bandari ya Pangani wilayani pangani mkoani Tanga.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Waziri Mbarawa amesema kuwa ujio wa kivuko hicho utafungua fursa za
kibiashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi wilayani hapo.
“Naamini ujio wa kivuko hiki
utarahisisha huduma za kijamii na maendeleo ya kiuchumi wilayani hapa,
hivyo naomba mkitunze vizuri kivuko hiki ili kiweze kudumu kwa muda
mrefu”, amesema Prof.Mbarawa.50 242
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha
huduma za kivuko zinakuwepo muda wote wilayani hapo, Serikali kupitia
Wizara hiyo imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa boti ambayo itatumika
kama mbadala wa usafiri wakati wa usiku katika maeneo hayo ambapo kivuko
cha Mv.Tanga hakifanyi kazi.
Kuhusu ujenzi wa Gati ya bandari
ya Pangani Waziri Mbarawa ameseama kuwa ujenzi wa gati hiyo utapelekea
Meli kubwa kuweza kutia nanga na kurahisisha usafiri wa moja kwa moja
kutoka Pangani kwenda visiwa vya Unguja na Pemba.
Amefafanua kuwa Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wataanzisha huduma ya boti za haraka
kutoka Pangani kwenda Mkokotoni Zanzibar hivyo kufungua fursa za
kibiashara na kitalii baina ya Tanga na Zanzibar.
Kwa upande wa huduma za
mawasiliano ya simu wilayani hapo, Prof.Mbarawa amesema kuwa huduma hiyo
itaanza mwezi Desemba mwaka huu kwa mkandarasi kufika na kuanza ujenzi
wa miundombinu ya simu na hivyo kuondoa tatizo la mawasiliano wilayani
hapo.
Katika hatua nyingine Prof.
Mbarawa amehahidi kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani-Saadani
hadi Bagamoyo (KM 242) kwa kiwango cha lami ifikapo mwakani.
Amefafanua kuwa ujenzi wa barabara
hiyo utakuwa wa awamu ili kuweza kuharakisha kukamilika kwake ambapo
awamu ya kwanza itahusisha kipande cha barabara ya Tanga- Pangani (KM
50) na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utafungua fursa za kiuchumi
kati ya Tanga na Pangani.
“Naahidi kujenga barabara hii
ambayo ni kiungo kati ya Tanga na Pangani, naamini ukamilifu wake
utalete maendeleo mkoani hapa”. Amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Eng.Joseph Nyamhanga amezipongeza kampuni za Songoro Marine
na Alpha Logistic kwa kumaliza kwa wakati ujenzi wa kivuko na Gati ya
bandari hiyo.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng.Manase Ole-kujan amesema kuwa kivuko
cha Mv.Tanga kimejengwa kwa sh.bilioni nne ambapo kina uwezo wa kubeba
tani 50 abiria 100 na magari madogo 6 kwa wakati mmoja.
Ujenzi wa Kivuko cha Mv. Tanga ni
moja ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli
aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani
Pangani Mkoani Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni