Ijumaa, 30 Septemba 2016

UVCCM WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI KWA KUWACHUKULIA HATUA MAOFISA WAKE KAGERA


bk4
Na Mwandishi Wetu
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umepongeza hatua  zilizochukuliwa na serikali kuwasimamaisha kazi, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani maofisa watano wanaotuhumiwa kufungua akaunti bandia kwa lengo la kuiba fedha za michango ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Umoja huo umesema  mashirika mengi ya umma, taasisi za serikali, viwanda na kampuni zilizoanzishwa wakati werikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati  Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kujenga uchumi na kutanua wigo wa ajira  vilikufa kwa uzembe.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kaimu katibu huyo mkuu alisema ili nidhamu ya uwajibikaji serikalini iweze kuzingatiwa haukana namna nyingine zaidi ya kuwawajibisha wanaokiuka utaratibu na kutengeneza njama za kula fedha zinazotengwa kwa ajili ama ya maendeleo au kusaidia wenye shida kama waathirika wa tetemeko hilo.
Alisema UVCCM inampongeza Rais Dk. John Magufuli na serikali yake na kuitia shime isirudi nyuma badala yake itimiza majukumu na wajibu wa kikatiba na kisheria bila kumfumbia macho mtumishi, kiongozi au hata mzee ambaye huko nyuma alishiriki kwenye ufisadi au uovu.
“UVCCM inavipongeza vyombo vya dola kuwafikisha mahakamani aliyekuwa Ofisa Tawala Mkoa (RAS) wa Kagera, Amantius Msole, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin Makonda, aliyekuwa Mhasibu wa Mkoa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB Kagera, Karlo Sendwa,”alisema.
Shaka  alisema kwa kuwa watuhumiwa hao wako mahakamani, UVCCM inaamini utaratibu wa kisheria utachukua mkondo wake. Mahakama ni eneo la utoaji haki, anayetuhumiwa kwa kesi huweza kuingizwa hatiani kwa mujibu wa sheria, kuachiwa huru au kuhukumumiwa  bila shinikizo lolote.
“Utendaji wa serikali katika dhamira ya kukuza dhana ya uwajibikaji, uadilifu, uzalendo na uwazi, usibaki serikalini pekee, UVCCM tunaahidi kila panapo na uchafu ndani ya jumuia kama wizi, ubadhirifu au ukwapuaji wa mali tutapekuwa, watakaobainika watachukuliwa hatua,”alisema.
Shaka alisema juhudi za serikali ya awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Nyerere zilipotea kutokana na waliokabidhiwa dhamana kutotimiza wajibu na kusababisha kampuni, viwanda na mashirika ya umma kufilisika na kufa kabisa jambo alilosema halipaswi kujirudia kwenye awamu hii ya sasa.
Alisema serikali ya Mwalimu Nyerere ilianzisha kampuni  za umma ikiwemo Aisco, Gapesco, BET, Kioo, Nedco, Bhesco, Napoco, Narco, Dafco, Dapco, Tacoshil na Nasaco ambazo zote zimekufa na waliozisababishia kufa wakiendelea kula maisha mjini bila ya kuchukuliwa hatu.
“Badala yake tukashuhudia walioongoza aidha taasisi, kampuni , viwanda na mashirika ya umma wakitamba na kujenga makasiri ya kifahari, kumiliki magari na miradi isiyolingana na vipato vyao halali,”alisema Shaka.
Alisema serikali ilifanikiwa kuanzisha na kuvisimamia viwanda mbalimbali kikiwemo Urafiki, Sungura Textile, Mutex, Ufi, Kizaku, viwanda vya kabungua korosho  Dar es salaam, Mtwara na Pwani,  Fishnet, Mtibwa Sugar na Kilombero ambavyo vilizalisha bidhaa tofauti kama Super Ghee, Pride, sabuni za Kodrai na Mbuni na Garnenia, mafuta ya kula yatokanayo na karanga, alizeti na Pamba.
Shaka alisema mashirika kama Shirika la Mabasi ya Taifa (KAMATA) na Usafiri Dar es Salam (UDA) ambayo hivi sasa ama hayapo au ufanisi wake ni duni kampuni za uchukuzi mikoani kama Kauru, Moretco, Kauma, Shirika la Reli yaliweza kumiliki mali mbalimbali ambazo kwa sasa hazipo.
“Yako wapi yote haya, tulikuwa na Shirika la Usafirishaji Mikoani (UMITA), kiwanda  cha viatu Bora, viwanda vya ngozi na beteri National. Vyote sasa  havipo, tujiulize  vilikwenda wapi, vilisibiwa na nini, kina nani walivihujumu, je walifikishwa mahakamani?”alihoji Shaka.
Alisema UVCCM inaunga mkono kinachofanywa sasa na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa itafanikisha mkakati wa taifa kuwa la viwanda kwa kuwa aina ya viongozi wadokozi na walafi ndio waliolirudisha nyuma taifa.
Aidha, Shaka alimuomba Rais Magufuli kutowaonea haya baadhi ya wanasiasa wakongwe wakiwemo waliowahi kushika nafasi nyeti na kusababisha madhara mbalimbali lakini sasa wamekuwa wakijitokeza hadharani na kupinga juhudi zake za kudhibiti uhujumu kama uliowahi kutokea.
“Hawa wazee ni matata kwani badala ya kuwatia moyo viongozi wachapakazi na wazalendo wamekuwa wakiwavunja moyo. waache upekepeke na kutomuunga mkono Rais Dk Magufulikama yaliwashinda waliokuwa kwenye nyadhifa basi wasiwe sababu ya kulazimisha kutolewa kwa nafasi ili yaendelee kufanyika hivi sasa” alisema.

WAZIRI MKUU APOKEA MICHANGO YA SH. MILIONI 190

koba1

 Baadhi ya watu walioshiki katika tukio la kukabidhi  jumla ya shilingi 190  ukiwa ni mchngo wa   waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kupokea mchngo huo kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
koba2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Tasisi ya Aga khan nchini, Amin Kurji (kulia) ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na wapili kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
koba3
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Balozi wa Pakistan nchini, Amir Khan  (wapili kushoto ukiwa ni mchango  kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani  Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na  kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
koba4
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. milioni 190 kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan.
Fedha hizo zimetolewa ili kusaidiia  wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.
Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali .
Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo (Ijumaa, Septemba 30, 2016) kwenye Hotel yaHyatt Regency jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri Mkuu aliwashukuru kwa michango hiyo na alitumia fursa hiyo kuwaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao.
“Ninawaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi kwa kuzileta ofisini kwangu au kutuma kupitia akaunti ya maafa iliyofunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz,” amesema.
Amesema watu walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya kupokea michango ya maafa hayo ambazo ni 0768-196-669 (M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).
Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Balozi wa Pakistan, Mhe. Amir alisema wanaamini mchango huo wa sh. milioni 80 walioutoa utasaidia kuwapunguzia uchungu wananchi wa Kagera kutokana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China Mhe. Haodong alimweleza Waziri Mkuu kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari walishawapeleka madaktari na wataalamu wengine mkoani Kagera na leo walikuwa wanakamilisha ahadi yao ya kutoa mchango wa sh. milioni 60.
Naye Muwakilishi Mkazi wa Taasisi za Aga Khan nchini, Amin Kurji  alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 50.

PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA BARABARA YA JUU KUKAMILIKA KWA WAKATI.


pea1
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale(Wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya ramani ya Ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover) kwa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa( Wa kwanza kushoto) wakati alipokagua ujenzi  huo Jijini Dar es salaam.
pea2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (Kulia kwake) wakati alipokagua ujenzi wa barabara za maingiliono (Tazara Flyover, Jijini Dar es salaam.
pea3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akifafanua jambo mara baada ya kukagua daraja la wapiti kwa miguu lilopo Buguruni Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa barabara wa Wizara Eng. Light Chobya.
pea4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Wananchi  mara baada ya kumaliza kukagua daraja la wapiti kwa miguu lililopo Buguruni Jijijni Dar es salaam.
…………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa  ameitaka Kampuni ya kikandarasi ya Sumitomo Mitsui inayojenga mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara kumaliza ujenzi huo kwa wakati mradi huo ili kusaidia kupunguza tatizo la msongamano.
Akizungumza mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutajenga historia  nchini kutokana na kuwa ni wa mwanzo kujengwa.
“Nimefurahi kuona mradi huu upo katika hatua nzuri, naomba mkamilishe mradi huu unakamilika kwa ubora na kwa wakati ili tatizo la msongamano lililopo katika maeneo haya kupungua au kuisha kabisa”, amesema Waziri Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa  umakini na kwa uangalifu wakati wa kipindi chote cha ujenzi ili kuitokuweza kusababisha foleni katika eneo hilo.
Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili kurahisisha kazi za ujenzi huo kukamilika kwa wakati na kupata matokeo chanya.
“Nawaomba watanzania wenzangu kuwa wavumilivu na usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote, kwani ukamilifu wa mradi huu utasaidia kupunguza tatizo la msongamano katika barabara hizi”, amefafanua Waziri Mbarawa.
Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amekagua daraja la watembea kwa miguu eneo la Buguruni Sheli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitunza daraja hilo ambalo uwepo wake umesaidia kupunguza ajali katika maeneo hayo.
“Ni matumaini yangu sasa wakazi wa maeneo  haya mtavuka kwa amani kupitia daraja hili, na ajali zilizokuwa zikitokea maramara hazitakuwepo tena”’, amesema Profesa Mbarawa.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemuahidi Waziri huyo kumaliza kwa wakati ujenzi huo na kumhaakikishia Waziri kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa na viwango vilivyo bora.
Mradi wa Tazara Flyover ni msaada kutoka Serikali ya Japan ambao umegharimu shilingi bilioni 93.4 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUFANYIKA TAREHE 1/10/2016


index
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatoa taarifa kuwa, tarehe 1 Oktoba ya kila mwaka, ni kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani. Katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku hii kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 49 la mwaka 1991. 
Maadhimisho ya siku ya wazee duniani ni moja kati ya jitihada za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) katika kutambua na  kuhamasisha jamii kuweza kulinda na kutetea haki za wazee duniani kote.  Umoja wa Mataifa umetenga siku hii kwa lengo la kutafakari hali ya maisha ya wazee na changamoto zinazowakabili wazee; na hivyo kuweka mipango thabiti ya kuboresha maisha yao na kuwafanya waishi maisha ya heshima, hadhi, na kuthaminiwa utu wao. 
Kila mwaka, Maadhimisho haya huwa yanabeba Kauli Mbiu yenye ujumbe mahsusi. Kwa mwaka 2016 Kaulimbiu inasema “Zuia Unyanyasaji dhidi ya Wazee”. Kaulimbiu hii inahimiza Serikali, jamii, na wadau wengine kutafakari na kuweka mikakati ya kukabiliana na vitendo vya ukatili, mauaji, ubaguzi na dhuluma dhidi ya wazee; vitendo ambayo ni kinyume dhidi ya haki za binadamu.
Maadhimisho haya kwa mwaka 2016 yanafanyika Kitaifa katika wilaya ya Mbalali, mkoani Mbeya. Kilele cha maadhimisho haya kitajumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo huduma ya upimaji wa hiari wa afya na ushauri kwa wazee, michezo na maonesho ya bidhaa na kazi mbalimbali zinazofanywa na wazee.
Katika kipindi hiki cha Maadhimisho hatuna budi kuenzi na kudumisha mila na desturi nzuri za kuwaenzi wazee kwa kutambua kuwa wazee ndiyo chanzo cha urithi wa historia ya nchi, washauri wa familia na jamii, watu wenye hekima, na walezi katika jamii. Hivyo jamii inaowajibu wa kuwaondolea vikwazo wazee katika kupata huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua pale ambapo mzee ananyanyashwa au kutendewa isivyostahili.
Erasto T. Ching’oro
Msemaji wa Wizara
30/9/2016

TFS YASAIDIA MADAWATI 12,000 MKOANI MWANZA

 tf2

Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika Mkoani Mwanzan jana  na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani  kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongela  ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .                 ( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii)
tf3
Naibu  Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Eng.  Ramo Makani( kushoto)  akimkabidhi  madawati  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ( kulia) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000,  wa  pili kushoto  ni Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii)
tf1
…………………………………………………………………………..
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imekabidhi madawati 12,115 mkoani Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000.
Makabidhiano hayo baina ya TFS na Serikali yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.
Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo , Ramo Makani alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kuhakikisha unakamilisha kutengenenza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya novemba mwezi huu
‘’ Pamoja na kufikia asilimia 61 ya lengo, nawaomba TFS muhakikishe idadi iliyobaki ya madawati inakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao’’ Alisema Makani.
Akizungumza kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo bila kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100 ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na kuwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa taratibu za uvunaji mbao katika baadhi  ya misitu.
TFS tumetekeleza agizo hili kwa kulenga ngazi za chini kabisa za mfumo wa utendaji wa Wakala  ambao ni wilaya. Hivyo katika kugawa idadi ya utengenezaji madawati wa kanda ilizingatia idadi ya wilaya kwa kila kanda’’ alisema Prof. Silayo.
Waziri Makani alisema madawati hayo yatagawiwa katika mikoa ya Simiyu., Kagera, Mara,Geita na Mwanza ambayo itapokea madwati 2,580 yaliyokwisha tengenezwa.
Akizungumz kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela aliwapongeza TFS na kuahidi kuyatunza madwati hayo ili yatumike kwa muda mrefu kwa manufaa ya wanafunzi.

Waziri Nape awatoa wasiwasi mashabiki wa soka kuhusu tiketi za kieletroniki.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)  leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016.
nna2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya upatikanaji  wa tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi  Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta.
nna3
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
nna4
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
nna5
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Mashabiki wa soka nchini wameondolewa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba na kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko vizuri na mpaka sasa tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
 Wasiwasi huo umetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri Nape amesema kuwa kuna kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo huu kutofanya kazi  katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi  kulalamika kukosa tiketi za mchezo wa kesho.
“kwa kila anayetaka kwenda uwanjani kesho kadi zinapatikana nimewaagiza Selcom wahakikishe wanazungusha  magari  yao mtaani  kuangalia  mahali penye upungufu na  yawe na watu wenye kadi hizo aidha,  watu waongezwe kwenye vituo ambayo vina idadi kubwa ya wateja wanaohitaji kadi” Alisema Mhe Nnauye.
Aidha Waziri Nape Nnauye amewahakikishia watanzania kuwa atausimamia mfumo huu kikamilifu na kwa gharama yoyote na  atahakikisha  hautakuwa  na mapungufu na endapo  yatajotokeza yatashughulikiwa na wataalamu ili kuufanya mfumo huu kufanya kazi ipasavyo kama ulivyokusudiwa.
 Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Selcom Tanzania Galius Runyeta  amefafanua kuwa mfumo huu uko wazi kabisa kwa wadau wote wanaohusika na mapato ya uwanjani na utakuwa  njia mbadala ya kudhibiti mapato yatokanayo na mechi.
“ Kwa mfumo huu hakuna njia ya mkato kila kitu kiko wazi na kwa kila dakika utaona mabadiliko ya idadi ya tiketi zinazonunuliwa na mpaka sasa zaidi ya tiketi 10,000 zimenunuliwa na zinazidi kununuliwa” Alisema Runyeta.
Kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuwepo kwa upotevu wa mapato katika mechi za ligi na kimataifa katika viwanja vya soka nchini kwa kuliona hilo Serikali iliamua kuanzisha mfumo utakaomaliza tatizo hilo na kukomesha mianya yote ya ulaji iliyokuwepo katika mfumo uliopita.

BENKI KUU YA TANZANIA YASEMA PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 7.9


 Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa BoT, Victoria Msima, akimkaribisha  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (wa pili kushoto), kuzungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu mwaka 2015 Dar es Salaam leo.
 Taswira ya meza kuu katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma, Victoria Msima,Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki,  Kenedy Nyoni, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu na Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera za Kiuchumi, David Kwimbere.
3
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandshi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu ya mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki,  Kenedy Nyoni.
 Wapiga picha wakiwa kazini.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanahabari Samuel kutoka kituo cha Televisheni ya ESTV akiuza swali
………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ukuaji wa pato la Taifa umeongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015.
 
Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la Taifa kwa robo na nusu mwaka 2016.
 
Profesa Ndulu alisema shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika kipindi hicho ni usafirishaji na uhifadhi wa mizigo ikiwa ni asilimia 30.6, uchimbaji wa madini kwa asilimia 20.5, mawasiliano na habari asilimia 12.6 na sekta ya fedha na bima kwa asilimia 12.5.
 
Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na uhifadhi wa mizigo umetokana na kuongezekea kwa usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara na gesi asilia ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.
 
“Kwa upande mwingine, ukuaji wa sekta ya uchimbaji wa madini na gesi umechangiwa zaidi na kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi ambao umekua kutoka mmSFt3.7,793 kwa mwaka 2015 mpaka mmSFt3 11,267 kwa mwaka 2016” alisema Ndulu
 
Profesa Ndulu alitaja sekta nyingine ambayo imefanya vizuri ililinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 kuwa ni sekta ya kilimo ambayo imekua kwa asilimia 3.2 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 wakati mwaka jana ilishuka kwa asilimia 1.9.
 
Aidha sekta ya fedha na bima imekua kwa asilimia 12.5 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 10.0 kwa robo ya pili ya mwaka 2015.
 
Akizungumzia ukuaji wa pato la Taifa alisema katika nusu ya mwaka 2016 yaani Januari hadi Juni 2o16 kasi ya ukuaji wa pato la taifa imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.
 

WAZIRI NAPE AKUTANA NA BALOZI WA SPAIN NCHINI.spa1

Waziri wa Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda kuhusu kusaidia kuendeleza sekta ya Utamaduni na Michezo leo Septemba 30,2016 wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwa Waziri  Jijini Dar es Salaam kukabidhi moja ya mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanywa na serikali ya Spain katika Bonde la Ufa la Olduvai Gorge Mkoani Manyara.
spa2
Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kuhusu kuendeleza mradi wa kujenga Shule ya Mpira wa Miguu Kigamboni kama ilivyokuwa katika mkakati wa awali alipofika Ofisini kwa waziri Jijini Dar es Salaam  Septemba 30, 2016 kumkaribisha kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Utamaduni yaliyoandaliwa na nchi ya Spain yatakayofanyika Makumbusho ya Taifa.
spa3
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akisoma mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanyika Olduvai Goerge mkoani Manyara baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
spa04
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) walipokuwa wakifanya mazungumzo Ofisini Jijini Dar es Salaam kuhusu kuendeleza sekta ya Utamaduni na Michezo Septemba 30, 2016.

Ijumaa, 23 Septemba 2016

MWENGE WATEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI NANE WILAYANI SINGIDA

indexMiradi ya maendeleo 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 8,391,131,054 imetembelewa na mwenge wa uhuru katika halmashauri za manispaa na singida wilayani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema miradi hiyo imejikita katika sekta za afya, maji, elimu, barabara, kilimo, ufugaji, miradi ya akina mama na vijana pamoja na vilabu vya wapinga rushwa na madawa ya kulevya.
Tarimo amesema katika halmashauri ya manispaa miradi iliyowekewa mawe ya msingi ni pamoja na stendi mpya ya mabasi yaendayo mikoani ambapo mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 3,726,072,678 na mradi wa barabara ya kiwango cha lami wenye thamani ya bilioni 2,694,339,096.
Aidha katika upande wa kuwajengea uwezo vijana kiuchumi manispaa imeendelea kutenga asilimia kumi ya bajeti ya mwaka ili kuwawezesha vijana mafunzo ya namna ya kubuni miradi na kuiendeleza.
Katika mapambano dhidi ya Ukimwi Tarimo amesema manispaa imeweza kuanzisha vituo kumi vya kupima Ukimwi na kutoa ushauri nasaha, vituo 26 vya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa motto na vine vya kutoa dawa za kufubaza VVU.
Amesema kwa kipindi cha Januari 2015 mpaka septemba 2016 wakazi wa manispaa 19,591 wamepima VVU ambapo waliopatikana na maambukizi ya VVU ni 1,124.
Kwa upande wa ugonjwa wa maralia ambapo kauli mbiu yake ni “wekeza katika maisha ya baadaye tokomeza maralia” manispaa imefanikiwa kupunguza maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo kutoka asilimia kumi mwaka 2014 hadi asilimia 3.7 mwaka 2015 kutokana na juhudi za manispaa za kutoa elimu ya kuteketeza mazalia ya mbu na matumizi ya vyandarua vilivyowekewa da ya viuatilifu.
Tarimo amefafanua kuwa wananchi wanaelimishwa na kushauriwa kuwahi hospitali pindi wanapoona dalili za homa na si kujinywea dawa bila maelekezo ya wataalamukwani si kila homa ni malaria na endapo watagundulika kuwa na ugonjwa wa malaria wanashauriwa kutumia dawa mseto na kukamilisha dozi.
Kwa upande wa halmashauri ya singida, mwenge wa uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi minane yenye thamani ya milioni 989,039,279 ambapo nguvu ya wananchi ni shilingi milioni 84,186,600, halmashauri ya wilaya ni milioni 21,607,450,  wahisani ni  76,742,000 na serikali kuu 806,503,229  pamoja na kuhamasisha wananchi juu ya umoja, mshikamano na uzalendo.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji wa kijiji cha Itaja wenye thamani ya shilingi milioni 411,405,887 uliokamilika mwezi Mei pamoja na miundombinu ya nyumba ya mashine, ufungaji wa jenereta na pamu za kusukumia maji, ujenzi wa njia kuu ya kupeleka maji kwenye matanki na ujenzi wa mtandao wa kusambaza maji kwenye vituo vya kuchotea maji.
Mradi huo utakaonufaisha wakazi wa Itaja kwa kuwapatia maji safi na salama umekabidhiwa kwa jumuiya ya watumia maji iliyopewa mafunzo ya uendeshaji na iko chini ya uangalizi kwa kipindi cha miezi sita.
Naye Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima ameweka jiwe la msingi ujenzi wa kiwanda cha kusindika mbogamboga kijiji cha msange na kuwashauri wanakikundi kuendeleza usindikaji wa mazao hayo kwani ni changamoto kwa wakulima kutokana na kuharibika haraka.
Amesema mradi ukisimamiwa utakuwa mkombozi wa wakulima kutokana na kuwa wakulima wengi hulalamika kuharibika mazao kutokana na kukosa masoko haraka hasa kwa mazoa ya mbogamboga, aidha mradi utatengeneza ajira kwa vijana na akina mama wengi wa kijiji cha msange na halmashauri ya Singida.
Ameongeza kwa kusisitiza kuwa mradi utaboresha afya ya wanajamii wanaouzunguka na kuwashukuru wahisani waliotoa shilingi milioni 47,000,000, huku halmashauri ikichangia milioni 2,000,000 na wananchi milioni 4,046,000 katika kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.
Miradi mingine iliyotembelewa na mwenge wa uhuru halmashauri ya Singida ni pamoja na klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Mughamo, mradi wa vijana wa ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira kijiji cha Msikii, Mradi wa utunzaji wa mazingira sekondari ya Mrama, ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mwahango na ujenzi wa ghala la kuhifadhia alizeti Kata