 Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha 
mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi 
Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 
27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu..
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha 
mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi 
Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 
27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu..Msiba upo nyumbani kwake eneo la Kisasa, Mjini Dodoma. Taarifa zaidi na taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na ratiba kamili ya maziko zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu pindi mipango itakapokamilika.
Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, amin!
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
27.11.2015
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni