WASHINDI WATATU WAKABIDHIWA TOYOTA( IST)LEO
Na Tinah Reuben,
Tuna furaha kupata nafasi ya
kubadilisha maisha ya watu kwa kuwapatia washindi magari aina ya Toyota (IST)"amesema Mkurugenzi Rasilimali Watu,Patrick Foya.
Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel imeendelea kutoa zawadi ya magari kwa washindi wa droo ya Yatosha.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi magari matatu leo jijini Dar
es salaam wakati akikabidhi zawadi za magari kwa washindi wa droo ya Yatosha
zinazoendelea kuchezeshwa na Kampuni ya Airtel .
Aidha alisema kwa sasa
takribani wateja 31 wamejishindia magari na amewataja washindi wliopata zawadi
ya gari kuwa ni,Habibu Shabani Mazome (mkazi wa Yombo),Fatema Hussein Mawji na
Emma Mkede Mosha(Mwalimu wa Shule ya Sekondari Jitegemee).
Amesisitiza watu kuendelea kutumia vifurushi vya
Yatosha ili waweze kupata nafasi ya kuibuka washindi kwani mtu yeyote anaweza
kuwa mshindi.
Mkurugenzi Rasilimali Watu,Patrick Foya(kushoto)na kulia ni Jackson Mbanda Afisa Uhusiano Airtel wakizungumza na Waandishi katika ugawaji zawadi leo jijini Dar es Salam.
Mshindi wa Toyota IST, Habibu Shabani Zome akikabidhiwa funguo ya gari aliyozawadiwa na Airtel.
Mshindi Emma Mkede Mosha akiweka saini baada kukabidhiwa gari.
Mshindi Fatema Hussein Mawji akiweka sainibaada ya kukabidhiwa gari.
Hapa Emma akikabidhiwa funguo.
Fatema akipokea funguo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni