Na Tinah reuben,
Asasi isiyokuwa ya Kiserikali (SVF)inayojighulisha na kusaidia watu wenye mahitaji maalum na waliosahaulika kama, walemavu na watu wanaoishi katika mazingira magumu Tanzania, imesema watu wenye ulemavu wako milioni 4.5 na kwamba wanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na mazingira wanayoishi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa shirika hilo ,Leontine Rwechungura amesema wanatambua mahitaji ya kundi la watu wenye ulemavu na wataanza kujenga miundombinu rafiki kwa wanafunzi katika shule za Sekondari, Pugu,jangwani na shule ya msingi mchanganyiko.
Amesema nusu ya watu wenye ulemavu hawapati elimu kama wanavyostahili,hivyo wakijengewa mazingira rafiki wanaweza kuondokana na changamoto na taifa kupata wataalam wanaotokana na kundi hilo.
“Kama taasisi tunawajibu wa kufanya na kila mmoja aweze kufanya kwa nafasi yake kutokana na wote ni jamii moja kwani mtu yeyote anaweza kupata ulemavu”alisema Rwechungura.
Pia Mwakilishi wa Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam ,Benardetha Thomas ameisisitiza asasi hiyo kufanya vitu ambavyo imeahidi kutokana na watu wengine wanaahidi na hawatekelezi.
Mwenyekiti wa Save Vulnerable Foundation (SVF),Fredy Kaula akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es saalam.
Katibu Mkuu wa SVF,Leontine Rwechungura akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwakilishi kutoka ofisi ya Afisa Elimu Mkoa Bearnadetha Thomas akitoa baadhi ya maelezo katika mkutano huo leo jijini Dar es saalam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni