KAIMU
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Inspekta Prisca Komba, ameibuka mshindi
wa Tuzo ya Mwanamke mwenye Mafanikio Tanzania kwa mwaka 2014.
Inspekta
Komba, ambaye pia anasimamia Dawati la
Jinsia kwenye mkoa huo wa Kipolisi, pia alishinda Tuzo ya Mwanamke wa Mwenye
Mafanikio katika Sekta ya Umma.
Wengine
waliopata tuzo mbalimbali ni pamoja na Debora Mwenda, aliyepata tuzo ya
Mwanamke mwenye mafanikio ya maisha, Penina Mlama, alipata tuzo ya Utamaduni na
Sanaa, Mary Gitanho, Tuzo ya Ustawi wa Jamii.
Sharmillah
Bhatt, tuzo ya Sayansi na Teknolojia, Jennifer Shigoli, tuzo ya Mwanamke mdogo
mwenye Mafanikio, Blandina Sembu, tuzo ya Habari na Mawasiliano.
Pia Dk.
Wineaster Anderson, tuzo ya Taaluma, Nahida Esmail, tuzo ya Elimu, Devotha
Likokola, Biashara na Ujasiriamali, Jacqueline
Mkindi, tuzo ya Kilimo, Mpendwa Chihimba,tuzo ya Afya na Angel Eaton, tuzo ya Michezo.
Tuzo hizo,
zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Tuzo za Wanawake Wenye
Mafanikio Tanzania (TWAA) inayoandaa tuzo hizo zilizokutanisha wanawake zaidi
ya 700.
Rais na Mwandaaji wa tuzo hizo, Irene Kiwia,
akikabidhi tuzo hizo alisema jumla ya
Wanawake 36 waliingia tatu bora katika vipengele 12 vilivyokuwa vinashindaniwa
na kati ya hizo jumla ya tuzo 14 zimetolewa.
“Katika
kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo inafanyika kitaifa kesho (leo) tumeona ni vyema tukawapatia tuzo
wanawake ambao wameleta mabadiliko chanya ndani ya jamii,kwani mafanikio yao
yanaleta hamasa kwa wanawake wengine wenye malengo,”alisema Kiwia.
Alivitaja
vipaumbele vya mwanamke ambaye anataka kuleta mabadiliko ndani ya jamii kuwa ni
ndoto,uthubutu,kufuatilia ndoto,uvumilivu na ustahimilivu.
Akizungumzia
tuzo hiyo, Ispekta Komba, ameishukuru jamii kwa kutambua umuhimu na kazi ambazo
amekuwa akizifanya ndani ya jamii na kwamba amepata nguvu ya kuendelea kufanya
kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.
“Sikutegemea
kupata tuzo hii na nimelia kwa chozi la furaha,namuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania (IGP), Ernest Mangu, pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias
Chikawe, kutoa vyeo kwa wakati ili kuongeza motisha wa kufanya kazi,”alisema
Komba
Aliitaka
serikali na mahakama kuhakikisha inasimamia kesi za udhalilishaji na ukatili wa
kijinsia zinatolewa hukumu mapema ili kumaliza vitendo hivyo ndani ya jamii na
pia kupunguza kasi ya udhalilishaji ambayo inatokana na watuhumiwa kutochukuliwa
hatua kwa wakati.
Pichani ni Raisi wa Taasisi ya Tuzo ya Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania ( IRENE KIWIA) akizungumza leo katika Utoaji wa tuzo hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam. |
Sharmillah Bhatt, Kushoto akipokea tuzo ya Sayansi na Teknolojia katika ukumbi wa Serena Hotel Leo Jijini Dar es salaam. |
KAIMU Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Inspekta Prisca Komba kushoto na kulia ni Irene Kiwia, Raisi wa tuzo za wanawake wenye mafanikio. |
Baadhi ya wahudhuriaji katika tuzo ya Mwanamke Mwenye Mafanikio Tanzania wakifuatilia utolewaji wa tuzo hizo. |
KAIMU Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Inspekta Prisca Komba, Msimamizi Dawati la Jinsia,akishangilia baadaya kushinda Tuzo ya Mwanamke wa Mwenye Mafanikio katika Sekta ya Umma. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni