Jumatano, 4 Machi 2015

SERIKALI YATAKIWA KUJENGA MFUMO MLENGO KWA MAENEO YA VIJIJINI

 Waigizaji wakiigiza katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika katika viwanja vya TGNP jijini Dar  es Salaam.

 Mkurugenzi wa TGNP,Lilian Liundi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya TGNP ,Jijini Dar es Salaam,
 Wanawake wakiwa na mabango yenye ujembe mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya TGNP ,Jijini Dar es Salaam

 Waziri  wa Kwanza mwanamke katika serikali ya awamu  ya kwanzaTabitha Siwale akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua maamaadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya TGNP ,Jijini Dar es Salaam

Na Tinah Reuben 
Serikali imekuwa ikitekeleza mlengo wa kijinsia katika maeneo ya  maeneo ya mijini na kuacha watu  wa maeneo ya vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto nyingi na kufanya watu hao kuendelea kuwepo kwa ukatili wa kijinsia.

Hayo ameyasema leo Tabitha Siwale wakati akifungua siku ya maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia nchini TGNP, uliofanyika katika viwanja vya mtandao huo jijini Dar es Salaam,amesema serikali itenge bajeti yenye mfumo wa mlengo wa kijinsia.

Tabitha ambaye alikuwa Waziri wa Kwanza mwanamke serikali ya awamu ya kwanza amesema pamoja na serikali kulidhia mikataba mbalimbali ikiwemo mkutano wa Berlin ukitaka upatikanaji wa viongozi ulitaka kuangalia mtazamo kijinsia.

Naye Mkurugenzi wa TGNP,Lilian Liundi  amesema serikali kuzingatia usawa wa kijinsia kwenye mchakato wa kupata viongozi ufikie asiliamia 50 kwa 50 itapunguza utofauti uliopo katika nafasi za juu za uongozi serikalini.

Aidha amesema kwa sasa kwenye nafasi zau kisiasa wanawake ni asilimia 30 kutoka asilimia nane mwaka 1995 hivyo serikali iendelee kutekeleza maazimio mbalimbali likiwemo la Baijing nchini China pamoja na maazimio ya milenia.

Hata hivyo,Lilian amesema pamoja na changamoto zilizopo katika utekelezaji wa azimio la pili ,tatu nane la milenia ambapo ni lazima seriakali kutekeleza katika kuweza kufikia malengo hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni