Jumapili, 1 Machi 2015

Ndege ya zamani ya Osama Bin Laden yashikiliwa Marekani

Ndege iliyokuwa ikimilikiwa na familia ya gaidi Osama Bin Laden inashikiliwa na polisi mjini Florida baada ya mmiliki wake mpya kushindwa kulipa deni la kununua ndege hiyo.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 22, aina ya Gulfstream II ina thamani ya dola za Marekani 4.5million (sawa na shilingi bilioni 8), ilikuwa ikitumiwa na famili ya Osama hadi mwaka 1980.
Hata hivyo, mmiliki wake mpya Jose Avelino Goncalves, 49, raia wa Venezuela anadaiwa kiasi cha dola milioni 3, ambazo alipaswa kumlipa mfanyabiasha mwenzake kwa makubaliano maalumu kuhusu ndege hiyo.
Goncalves anadaiwa na mfanyabiashara mwenzake,  Luis Enrique Nuñez-Villanueva kiasi cha dola milioni 3.
Katika makubaliano yao, Goncalves alidai kukubali kulipa kiasi cha dola 1.5 kama kianzio na kisha kulipa dola 500,000 kila mwezi hadi deni litakapokwisha.
Ndege hiyo ni chaguo la wafanyabiashara wengi matajiri kutokana na uwezo wake wa kusafiri mwendo mrefu ikiwa angani bila kushuka chini, lakini pia jinsi ilivyotengenezwa ni ya pekee kwa aina yake kati ya ndege  ndogo za kubeba abiria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni