Na Tina Reuben
Mkuu wa Wilaya ya
kinondoni Paul Makonda ameitaka Hospitali ya TMJ kushugulikia kwa haraka
urekebishaji wa bomba la kupitishia maji machafu yanayotoka katika Hospitali
hiyo kwani inaweza kusababisha madhara wakati wa mafuriko.
“Hospitali kubwa lakini
inajivunjia heshima kwa kuhindwakudhibiti mifereji ya maji machafu na licha ya
uchafu kuna kemikali ambazo zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kwa Wakazi
wanaoishi kwenye maeneo hayo.”
Makonda ameyasema hayo
leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kukagua barabara na mifereji
inayosaidia wakati wa mafuriko tunapopata taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya
Hewa Nchni(TMA)
Ametoa siku saba kwa
TMJ kushughulikia hilo wakishindwa hatua za kisheria zitafuatwa na amewataka
Wananchi kuacha kutupa taka katika eneo la mtaro kwani unasababisha kuziba kwa
kalawati linalopeleka maji hayo baharini na wanaochimba na kuchota mchanga
katika ukingo wamtaro kuacha mara moja.
“Nawaomba watu wanaoishi kwenye maeneo ya bondeni wahame
wasisubiri mpaka mvua zianze kunyesha na Wananchi wanaoishi jirani na eneo la
mtaro kushirikiana kwa pamoja katika kudhbiti utupaji taka kwenye eneo hilo.
Naye Mhandisi Mkuu wa
Manispaa ya Kinondoni Eng.Baraka Mkuya amesema wapo katika mradi wa kujenga
barabara ili kupunguza msongamano wa magari kwani eneo la Kinondoni linaongoza
kwa foleni lina muunganiko wa kutoka
Bagamoyo na Mkoa wa Morogoro.
Amezitaja barabara ni Chwaku,SerengetiJournalism,Sanya(inayounganisha
Mwai Kibaki na Ali Hassan Mwinyi) zote zimekamilika isipokuwaChwaku ambayo
imekwama kuendelea kujengwa kutokana na
mifumo maji taka inayoimamiwa na Shirika la Maji safi na Maji taka (DAWASCO).
Mkuya ametaja
changamoto inayowakabili ni mgogoro kati ya Manispaa na Shirika la maji Dar es
Salaam(DAWASCO)ambayo inataka kulipwa fidia kiasi cha milioni 139 ili kuhamisha
mitambo yao waliyoifunga.
Amesema hayo yanawapa
wakati mgumu katika utekelezaji wa kazi zao kwani Wananchi wanailalamikia Manispaa
kuwa haitekelezi hivyo kuwalazimu kuwalipa DAWASCO imeshalipa zaidi ya bilioni 1 ambayo
ni kinyume ch sheria ya mwaka 2007 inayowataka kuhamisha mitambo kwa gharama
zao na kuifunga maeneo watayoelekezwa na Manispaa kwa vibali maalum.
Vilevile ameyataja
mashirika mengine ambayo yako kwenye mgogoro huo ni Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)na
Shirika la Mawasiliano(TTCL).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni