Jumapili, 1 Machi 2015

Kanisa lanusurika kuchomwa moto

Kanisa la Pentekoste Tanzania Usharika wa Tandika, Manispaa ya Temeke limenusurika kuteketezwa kwa moto mwishoni mwa wiki iliyopita na polisi wanamshikilia mtu mmoja kwa madai ya kuhusika katika jaribio hilo lililoshindikana.
Mbali na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Zacharia Sebastian alisema mtuhumiwa huyo anatarajia kufikishwa mahakamani leo hii.
Hiyo ni mara ya pili kwa kanisa hilo kunusurika kuchomwa moto, likitanguliwa na lile la mwaka jana ambapo hadi leo kesi haijafikishwa mahakamani kwa madai ya kutokamilika kwa uchunguzi.
Raymond Noya, Askofu wa Kanisa Jimbo la Temeke alithibitisha kanisa hilo kunusurika kuchomwa na moto.
nao kwa chakula. Hakuna ugomvi wowote kati yetu. Hii inashangaza,” alisema John.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni