Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, ambaye amejiteua kuwa Balozi wa Kupigania Mauaji ya Albino, Bw. Henry Mdimu (wa pili kutoka kushoto) akiongea na waandishi wa habari kutangaza dhamira yake ya dhati ya kujitolea kutoa elimu kwa watu ili waweze kuacha mauaji. Pembeni wanaomzunguka ni kamati inayomuunga mkono ili kufanikisha harakati ya IMETOSHA.
(PICHA/HABARI NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG).
(PICHA/HABARI NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG).
Mwenyekiti wa Harakati ya IMETOSHA, Bw. Masood Kipanya akikazia jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii Cassim Mganga akisalimia na waandishi wa habari.
Mweka hazina wa mfuko wa harakati ya IMETOSHA, Bi. Monica akiongea machache.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia.
Wanaharakati ya IMETOSHA wakishow love.
Picha ya pamoja.
---
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Bw Henry Mdimu leo hii mchana amezungumza na vyombo vya habari kuvieleza azma yake ya kuendesha harakati mpya iitwayo IMETOSHA kupinga ukatili na mauaji dhidi ya albino.
Akizungumza katika Ukumbi wa Idara maelezo jijini Dar es Salaam, Mdimu alisema kuwa harakati yake imelenga zaidi katika kuelimisha jamii kuwa albino ni binadamu kama wengine na wanahaki ya kutonyanyapaliwa, kusemwa vibaya, kutemwa mate, kukatwa viungo na kuuawa.
Balozi Mdimu alieleza azma ya kamati yake ya kuandaa matembezi ya hisani yanayitarajia kufanyika Jumamosi ya Machi 21, 2015 yatakayoanzia viwanja vya Leaders Club kuelekea Morocco, Manyanya, Kinondoni Road, Ali Hassan Mwinyi na hatimaye kuishia hapo hapo viwanja vya Leaders Club ambapo patafanyika mnada wa picha iliyochorwa na Ndunguru pia fulana zenye neno ya IMETOSHA zitauzwa pale ili kupatikane pesa ambazo Balozi Mdimu na kamati yake watazitumia kwenda Kanda ya Ziwa kufanya kampeni mijini na vijijini juu ya Mauaji na Manyanyaso dhidi ya ndugu zetu albino.
Pia Mdimu aliwapongeza rafiki zake ambao amekuwa nao bega kwa bega mpaka leo kwa kujitoa kufanikisha harakati yake mpaka sasa.
Aidha aliongeza kuwa baadhi ya wasani wakiwemo Jhikoman, Profesa Jay, Mwana FA, Cassim Mganga, Fid Q, Ray C na Roma wamejitolea kurekodi wimbo mmoja kila msanii ambapo album itauzwa kutunisha mfuko utakasaidia harakati ya IMETOSHA huko kanda ya Ziwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni