Jumanne, 10 Machi 2015

WAKAGUZI WA MABEHEWA MABOVU WA TRL KUCHUKULIWA HATUA

 Mabehewa yaliyoingizwa nchini kutokea Kampuni ya Malaysia yamebainika kuwa yako chini ya kiwango na hivyo wale ambao wamehusika na ukaguzi na kufanya mabehewa hayo yaingizwe watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,amesema Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta.
  

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara alipotembelea Shirika la Reli Nchini (TRL),Sitta alisema serikali ikidhibitika waliokagua na kudhibitisha kuleta mabehewa hayo watachukuliwa hatua.

“Nchi ni masikini hivyo wote waliohusika katika uingizaji wa mabehewa hayo watachukuliwa hatua za kisheria za nchi ikiwa ni pamoja na kusitisha mkataba  huo na hili nitalifuatilia kwa karibu na bodi ya TRL nimeiagiza kufanya hivyo”alisema Sitta.

Sitta alisema amezuia mabehewa 124 kutoka kwa watu walioingia mkataba na Kampuni ya TRL kutokana na kuingia kwa mabehewa yasiyokuwa na ubora Nchini. 

Pia alisema hali  shirika ni nzuri na mapato yake yameongezeka kutokana na watu kujipanga katika uendeshaji wa shirika hilo.  

 
 Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta akizungumza na waandishi hawapo pichani leo katika Mkutano na TRL leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Waandishi wakifuatilia wakichukua habari.


Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta akizungumza na wandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi,Monica Mwamunyange,kulia ni Naibu Waziri,Charles Tizeba.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni