Jumapili, 29 Machi 2015

SITTA AKAMILISHA MPANGO WA RELI MPYA (STANDARD GAUGE)

NA TINA RUBEN,
Waziri wa Uchukuzi,Samuel Sitta amesema  kuwa RAHCO (Kampuni ya Rasimali za Reli)wamekamilisha utaratibu  wa kumpata Mshauri wa Mradi  ambaye  ni Kampuni ya  Roths child ambayo  itawezesha kupata fedha za ujenzi wa Reli Mpya ya kati kwa Kiwango cha "Standard  Gauge "ambayo gharama yake ya ujenzi  ni Dola za Kimarekani Bilioni 7.6.
 
Alisema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari,amesema fedha hiyo ni  ni sawa na shilingi  za Kitanzania  Trilioni 14 reli hiyo  itakuwa na urefu wa Kilomita 2561.

Sitta alisema mradi huo utakuwa  mkubwa kutekelezwa  na serikali  toka tupate Uhuru,na Serikali  haitatoa hata dola Moja kutoka Hazina bali utagharamiwa na mabenki ambayo ndiyo yatakayotoa fedha.

 Reli hiyo Mpya kabisa tofauti  na  iliyopo itakuwa  yenye uwezo mkubwa wa Kimataifa "Standard Gauge railway " itaanzia Dar es Salaam Mpaka Kigoma, kupitia Tabora, Mwanza,Isaka hadi Rusumo; Kaliua -Mpanda -Karema na Uvinza -Musongati nchini Burundi.

 Pia alisema  reli hiyo itasaidia kukidhi mahitaji  makubwa ya ubebaji mizigo kwenda nchi jirani za DRC, Rwanda, Burundi,  na Uganda na itasaidia  Wananchi  kwenda mikoani kwa wingi na kwa kasi zaidi.

  "Wengi watajiuliza kwa nini tumeamua kujenga reli Mpya?
  Ni kutokana na sababu  kwamba reli  iliyopo sasa ambayo ni ya Kiwango cha "meter Gauge " uwezo wake  wa kubeba mizigo hata baada ya ukarabati kwa mwaka ni tani Milioni 5,ambazo haziwezi  kukabili mahitaji ya mizigo ya Kanda hii ambayo itafikia tani Milioni 30 ifikapo mwaka 2025".Alisema Sitta.

  
Mradi huu wa kujenga reli ya kati utaajiri watanzania takribani 300,000 watakaohusika na ujenzi  wa reli hiyo itakayojengwa kwa muda wa miaka 5 .Reli hiyo itafanya upelekaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam  Mpaka nchini DRC kuchukua muda wa takribani saa 12.

 "Tumejipanga ili Uzinduzi  wa ujenzi wa reli hii ya kihistoria  ufanywe na Mheshimiwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  kwa kuweka jiwe la msingi ifikapo tarehe 30 Juni , 2015 yaani Mwaka huu tulionao kule Mpiji Kituo cha stesheni Mkoa wa Pwani ambako ndiko reli itaanzia". Alisema

   Kwa ujumla reli zote  zitagharimu jumla ya kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 14.2 ambazo ni  sawa na shilingi za Kitanzania  Trilioni 26 zitaajiri  zaidi  ya watanzania  Milioni  Moja kwa miaka  yote zitakapokuwa zinajengwa.
 Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta akizungumza na waandishi leo ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari

Jumatano, 18 Machi 2015

NYALANDU AKABIDHIWA NDEGE

Wakiwa katika picha ya pamoja
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazari Nyalandu (kushoto) akikabidhiwa ndege aina ya Micro Light Nyinja, 5H-HEL, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utalii ya Tanganyika Wildlife Safari, Eric Pasanisi, werngine ni Askari wa kikosi cha wanyamapori walio hudhuria makabidhiano hayo.



Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa na Rubani wa ndege aina ya Micro Light Nyinja, muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ndege hiyo. Ndege hiyo ambayo imenunuliwa na kampuni ya Tanganyika Wildlife Safari ilikabidhwa kwa Waziri Nyalandu kwaajili ya kufuatilia majangili kwenye hifadhi za taifa.

Jumamosi, 14 Machi 2015

MAKONDA AWAPATA SIKU SABA TMJ

Na Tina Reuben


Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda ameitaka Hospitali ya TMJ kushugulikia kwa haraka urekebishaji wa bomba la kupitishia maji machafu yanayotoka katika Hospitali hiyo   kwani inaweza kusababisha madhara  wakati wa mafuriko.

“Hospitali kubwa lakini inajivunjia heshima kwa kuhindwakudhibiti mifereji ya maji machafu na licha ya uchafu kuna kemikali ambazo zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kwa Wakazi wanaoishi kwenye maeneo hayo.”

Makonda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kukagua barabara na mifereji inayosaidia wakati wa mafuriko tunapopata taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchni(TMA)

Ametoa siku saba kwa TMJ kushughulikia hilo wakishindwa hatua za kisheria zitafuatwa na amewataka Wananchi kuacha kutupa taka katika eneo la mtaro kwani unasababisha kuziba kwa kalawati linalopeleka maji hayo baharini na wanaochimba na kuchota mchanga katika ukingo wamtaro kuacha mara moja.

“Nawaomba watu  wanaoishi kwenye maeneo ya bondeni wahame wasisubiri mpaka mvua zianze kunyesha na Wananchi wanaoishi jirani na eneo la mtaro kushirikiana kwa pamoja katika kudhbiti utupaji taka kwenye eneo hilo.

Naye Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Eng.Baraka Mkuya amesema wapo katika mradi wa kujenga barabara ili kupunguza msongamano wa magari kwani eneo la Kinondoni linaongoza kwa foleni  lina muunganiko wa kutoka Bagamoyo na Mkoa wa Morogoro.

Amezitaja barabara ni Chwaku,SerengetiJournalism,Sanya(inayounganisha Mwai Kibaki na Ali Hassan Mwinyi) zote zimekamilika isipokuwaChwaku ambayo imekwama  kuendelea kujengwa kutokana na mifumo maji taka inayoimamiwa na Shirika la Maji safi na Maji taka (DAWASCO).
Mkuya ametaja changamoto inayowakabili ni mgogoro kati ya Manispaa na Shirika la maji Dar es Salaam(DAWASCO)ambayo inataka kulipwa fidia kiasi cha milioni 139 ili kuhamisha mitambo yao waliyoifunga.

Amesema hayo yanawapa wakati mgumu katika utekelezaji wa kazi zao kwani Wananchi wanailalamikia Manispaa kuwa haitekelezi hivyo kuwalazimu kuwalipa  DAWASCO imeshalipa zaidi ya bilioni 1 ambayo ni kinyume ch sheria ya mwaka 2007 inayowataka kuhamisha mitambo kwa gharama zao na kuifunga maeneo watayoelekezwa na Manispaa kwa vibali maalum.

Vilevile ameyataja mashirika mengine ambayo yako kwenye mgogoro huo ni Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)na Shirika la Mawasiliano(TTCL).

MAKONDA WAPA SIKU SABA TMJ

Mkuu wa Wilaya ya KInondoni Paul Makonda akikagua chemba ambayo inatoa maji kutoka Hospitali ya TMJ.


 Mkuu wa Wilya ya Kinondoni Paul Makonda(katikati)na(kulia)ni Mkandarasi wa Del Monte (T)ltd na kushoto ni Mhandishi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya leo jijini Dar es Salaam.

 Akizungumza na Wajumbe wa Kata ya Bonde la Mpunga Wilaya ya Kinondoni.


 Hili ndilo kalawati linalopeleka maji baharini.

 Wakianglia moja ya chemba zilizoziba.


Jumatano, 11 Machi 2015

WASHINDI WATATU WAKABIDHIWA TOYOTA( IST)LEO


 Na Tinah Reuben,

Tuna furaha kupata nafasi ya kubadilisha maisha ya watu kwa kuwapatia washindi magari aina ya Toyota (IST)"amesema Mkurugenzi Rasilimali Watu,Patrick Foya.

Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel imeendelea kutoa zawadi ya magari kwa washindi wa droo ya Yatosha.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi magari matatu leo jijini Dar es salaam wakati akikabidhi zawadi za magari kwa washindi wa droo ya Yatosha zinazoendelea kuchezeshwa na Kampuni ya Airtel .

 

Aidha alisema kwa sasa takribani wateja 31 wamejishindia magari na amewataja washindi wliopata zawadi ya gari kuwa ni,Habibu Shabani Mazome (mkazi wa Yombo),Fatema Hussein Mawji na Emma Mkede Mosha(Mwalimu wa Shule ya Sekondari Jitegemee). 

 

 

Amesisitiza watu kuendelea kutumia vifurushi vya Yatosha ili waweze kupata nafasi ya kuibuka washindi kwani mtu yeyote anaweza kuwa mshindi.                                                                                            

 Mkurugenzi Rasilimali Watu,Patrick Foya(kushoto)na kulia ni Jackson Mbanda Afisa Uhusiano Airtel wakizungumza na Waandishi katika ugawaji zawadi leo jijini Dar es Salam.

 Mshindi wa Toyota IST, Habibu Shabani Zome akikabidhiwa funguo ya gari aliyozawadiwa na Airtel.

 Mshindi  Emma Mkede Mosha akiweka saini baada kukabidhiwa gari.

 Mshindi  Fatema Hussein Mawji akiweka sainibaada ya kukabidhiwa gari.

 Hapa Emma akikabidhiwa funguo.

 Fatema akipokea funguo.

Jumanne, 10 Machi 2015

WAKAGUZI WA MABEHEWA MABOVU WA TRL KUCHUKULIWA HATUA

 Mabehewa yaliyoingizwa nchini kutokea Kampuni ya Malaysia yamebainika kuwa yako chini ya kiwango na hivyo wale ambao wamehusika na ukaguzi na kufanya mabehewa hayo yaingizwe watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,amesema Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta.
  

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara alipotembelea Shirika la Reli Nchini (TRL),Sitta alisema serikali ikidhibitika waliokagua na kudhibitisha kuleta mabehewa hayo watachukuliwa hatua.

“Nchi ni masikini hivyo wote waliohusika katika uingizaji wa mabehewa hayo watachukuliwa hatua za kisheria za nchi ikiwa ni pamoja na kusitisha mkataba  huo na hili nitalifuatilia kwa karibu na bodi ya TRL nimeiagiza kufanya hivyo”alisema Sitta.

Sitta alisema amezuia mabehewa 124 kutoka kwa watu walioingia mkataba na Kampuni ya TRL kutokana na kuingia kwa mabehewa yasiyokuwa na ubora Nchini. 

Pia alisema hali  shirika ni nzuri na mapato yake yameongezeka kutokana na watu kujipanga katika uendeshaji wa shirika hilo.  

 
 Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta akizungumza na waandishi hawapo pichani leo katika Mkutano na TRL leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Waandishi wakifuatilia wakichukua habari.


Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta akizungumza na wandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi,Monica Mwamunyange,kulia ni Naibu Waziri,Charles Tizeba.


Jumamosi, 7 Machi 2015

MWANAMKE BORA MWENYE MAFANIKIO AKABIDHIWA TUZO LEO MARCH, 7


KAIMU Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Inspekta Prisca Komba, ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mwanamke mwenye Mafanikio Tanzania kwa mwaka 2014.
Inspekta Komba, ambaye pia  anasimamia Dawati la Jinsia kwenye mkoa huo wa Kipolisi, pia alishinda Tuzo ya Mwanamke wa Mwenye Mafanikio katika Sekta ya Umma.

Wengine waliopata tuzo mbalimbali ni pamoja na Debora Mwenda, aliyepata tuzo ya Mwanamke mwenye mafanikio ya maisha, Penina Mlama, alipata tuzo ya Utamaduni na Sanaa, Mary Gitanho, Tuzo ya Ustawi wa Jamii.

Sharmillah Bhatt, tuzo ya Sayansi na Teknolojia, Jennifer Shigoli, tuzo ya Mwanamke mdogo mwenye Mafanikio, Blandina Sembu, tuzo ya Habari na Mawasiliano.

Pia Dk. Wineaster Anderson, tuzo ya Taaluma, Nahida Esmail, tuzo ya Elimu, Devotha Likokola, Biashara  na Ujasiriamali, Jacqueline Mkindi, tuzo ya Kilimo, Mpendwa Chihimba,tuzo ya Afya na Angel Eaton, tuzo ya Michezo.

Tuzo hizo, zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Tuzo za Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania (TWAA) inayoandaa tuzo hizo zilizokutanisha wanawake zaidi ya 700.

 Rais na Mwandaaji wa tuzo hizo, Irene Kiwia, akikabidhi tuzo hizo alisema  jumla ya Wanawake 36 waliingia tatu bora katika vipengele 12 vilivyokuwa vinashindaniwa na kati ya hizo jumla ya tuzo 14 zimetolewa.

“Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo inafanyika kitaifa  kesho (leo) tumeona ni vyema tukawapatia tuzo wanawake ambao wameleta mabadiliko chanya ndani ya jamii,kwani mafanikio yao yanaleta hamasa kwa wanawake wengine wenye malengo,”alisema Kiwia.

Alivitaja vipaumbele vya mwanamke ambaye anataka kuleta mabadiliko ndani ya jamii kuwa ni ndoto,uthubutu,kufuatilia ndoto,uvumilivu na ustahimilivu.

Akizungumzia tuzo hiyo, Ispekta Komba, ameishukuru jamii kwa kutambua umuhimu na kazi ambazo amekuwa akizifanya ndani ya jamii na kwamba amepata nguvu ya kuendelea kufanya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.

“Sikutegemea kupata tuzo hii na nimelia kwa chozi la furaha,namuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Ernest Mangu, pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, kutoa vyeo kwa wakati ili kuongeza motisha wa kufanya kazi,”alisema Komba

Aliitaka serikali na mahakama kuhakikisha inasimamia kesi za udhalilishaji na ukatili wa kijinsia zinatolewa hukumu mapema ili kumaliza vitendo hivyo ndani ya jamii na pia kupunguza kasi ya udhalilishaji ambayo inatokana na watuhumiwa kutochukuliwa hatua kwa wakati.




Pichani ni Raisi  wa Taasisi ya Tuzo ya Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania  ( IRENE KIWIA) akizungumza leo katika Utoaji wa tuzo hizo uliofanyika katika  Ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam.

 

Debora Mwenda Mwanahabari mkongwe wa Redio Tanzania  Akizungumza baada ya kupokea tuzo ya Mwanamke  mwenye mafanikio ya maisha, Akielezea ni jinsi gani alivyofanikiwa kuelimisha jamii kupitia kipindi chake cha (Mama na mwana) kilichokuwa kikirushwa hewani Redio Tanzania.

Sharmillah Bhatt, Kushoto akipokea tuzo ya Sayansi na Teknolojia katika ukumbi wa Serena Hotel Leo Jijini Dar es salaam.

KAIMU Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Inspekta Prisca Komba kushoto na kulia ni  Irene Kiwia,  Raisi wa tuzo za wanawake wenye mafanikio.

Baadhi ya wahudhuriaji katika tuzo ya Mwanamke Mwenye Mafanikio Tanzania wakifuatilia  utolewaji wa tuzo hizo.

KAIMU Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Inspekta Prisca Komba, Msimamizi Dawati la Jinsia,akishangilia baadaya  kushinda Tuzo ya Mwanamke wa Mwenye Mafanikio katika Sekta ya Umma.

  

Ijumaa, 6 Machi 2015

SERIKALI YA JAPAN YAIPATIA MSAADA WA DOLA LAKI 1.4 HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati alipowasili nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki Jijini Dar es salaam,kulikofanyika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) akionyesha kitu kwenye karatasi kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine,wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga akitoa hotuba yake mbele ya Ujumbe wa Wilaya ya Monduli pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakisaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Monduli.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.Wengine pichani ni Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine (katikati),Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Idara ya Miradi wa Ubalozi wa Japan nchini,Takashi Higuchi.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakibadilishana mikataba mara baada ya kuisaini,wakati wa hafla ya fupi iliyofanyika leo nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki jijini Dar.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri ya Monduli dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi miwili ya wilaya hiyo.Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine akitoa akizungumza machache mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga mara baada ya hafla hiyo.

Alhamisi, 5 Machi 2015

HENRY MDIMU AANZISHA HARAKATI DHIDI YA UKATILI NA MAUAJI KWA ALBINO

 Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, ambaye amejiteua kuwa Balozi wa Kupigania Mauaji ya Albino, Bw. Henry Mdimu (wa pili kutoka kushoto) akiongea na waandishi wa habari kutangaza dhamira yake ya dhati ya kujitolea kutoa elimu kwa watu ili waweze kuacha mauaji. Pembeni wanaomzunguka ni kamati inayomuunga mkono ili kufanikisha harakati ya IMETOSHA. 
(PICHA/HABARI NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG).
Mwenyekiti wa Harakati ya IMETOSHA, Bw. Masood Kipanya akikazia jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii Cassim Mganga akisalimia na waandishi wa habari.
Mweka hazina wa mfuko wa harakati ya IMETOSHA, Bi. Monica akiongea machache.
 Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia.
Wanaharakati ya IMETOSHA wakishow love.
Picha ya pamoja.
---
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Bw Henry Mdimu leo hii mchana amezungumza na vyombo vya habari kuvieleza azma yake ya kuendesha harakati mpya iitwayo IMETOSHA kupinga ukatili na mauaji dhidi ya albino.
Akizungumza katika Ukumbi wa Idara maelezo jijini Dar es Salaam, Mdimu alisema kuwa harakati yake imelenga zaidi katika kuelimisha jamii kuwa albino ni binadamu kama wengine na wanahaki ya kutonyanyapaliwa, kusemwa vibaya, kutemwa mate, kukatwa viungo na kuuawa.
Balozi Mdimu alieleza azma ya kamati yake ya kuandaa matembezi ya hisani yanayitarajia kufanyika Jumamosi ya Machi 21, 2015 yatakayoanzia viwanja vya Leaders Club kuelekea Morocco, Manyanya, Kinondoni Road, Ali Hassan Mwinyi na hatimaye kuishia hapo hapo viwanja vya Leaders Club ambapo patafanyika mnada wa picha iliyochorwa na Ndunguru pia fulana zenye neno ya IMETOSHA zitauzwa pale ili kupatikane pesa ambazo Balozi Mdimu na kamati yake watazitumia kwenda Kanda ya Ziwa kufanya kampeni mijini na vijijini juu ya Mauaji na Manyanyaso dhidi ya ndugu zetu albino.
Pia Mdimu aliwapongeza rafiki zake ambao amekuwa nao bega kwa bega mpaka leo kwa kujitoa kufanikisha harakati yake mpaka sasa.
Aidha aliongeza kuwa baadhi ya wasani wakiwemo Jhikoman, Profesa Jay, Mwana FA, Cassim Mganga, Fid Q, Ray C na Roma wamejitolea kurekodi wimbo mmoja kila msanii ambapo album itauzwa kutunisha mfuko utakasaidia harakati ya IMETOSHA huko kanda ya Ziwa.

WAFANYABIASHARA WAILALAMIKIA SERIKALI KUPANDISHA KODI BILA KUWASHIRIKISHA

Na Tinah Reuben
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Dar es salaam (JWT), Philimon Chonde amesema suala la kupandishwa kwa kodi kwa asilimia mia moja limepitishwa kinyemela bila ya wao kuwashirikisha wala kujadiliana na wafanyabiashara hao.
Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha wabunge, ameeleza kuwa mfumo wa kodi uliopo umekaa kikoloni kwani unawakandamiza wafanyabiashara ili waendelee kuwa tawala kwani haungalii uwiano uliopo baina ya wafanyabiashara wakubwa na wafanyabishara wadogo.
Chonde amesema kutokana na kuwepo kwa usumbufu wa kudai leseni ameitaka Serikali kuweka suala la kodi katika mfumo unaoeleweka ili kumsaidia mfanyabiashara kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa kwa mwezi.
Naye Mbunge wa Temeke Abasi Mtevu amezitaja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao ni suala la usafi wanalipia lakini mazingira bado ni machafu na wamesema wapo tayari kufanya usafi wenyewe na suala la zima moto kwamba kila mfanyabiashara aweze kuwa na mtungi wa gesi lakini hawapewi mitungi hiyo bali hupewa karatasi ya malipo.
Pia amesema sheria zinazopitishwa Bungeni baadhi ni kweli na nyingine zimetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi na amewasisitiza wafanyabiashara kupambana katika kulinda biashara pamoja na mitaji yao.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Dar es Salaam (JWT), Philimon Chonde akizungumza katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu akisisistiza jambo katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akifanya majumuisho katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wafanyabiashara akiombea mkutano kabla haujaanza.
 Mbunge wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akisalimia na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azan Zungu katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
 Waheshimiwa wabunge wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mkutano, kutoka kulia ni Mhe. Abbas Mtemvu, Mhe. John Mnyika na Mhe, Mussa Azan Zungu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
 Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria katika mkutano huo.