ZIARA ya Mbunge wa
Rufiji,Mohamed Mchengerwa,(CCM) imebaini uuzwaji wa ardhi iliyokuwa
imetengwa kwa ajili ya kiwanda cha sukari katika kijiji cha Chumbi
ambayo imeuzwa kwa hekari moja shilingi 10,000.
Baada
ya Mbunge huyo kufika katika mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi
na kusikiliza kero zao juzi katika kijiji cha Chumbi alikutana na kilio
cha eneo lenye ekari 2400 kuuzwa kwa shilingi milioni 24 pekee.
Wananchi
wa eneo hilo walimtaja Diwani wa Kata ya Chumbi ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumbi C,Salum Mtimbuko (CCM) kuwa ndiye
aliyeuza eneo hilo kwa muwekezaji ambaye anamjua mwenyewe na alipewa
Baraka zote na Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Njwayo.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapo,Mussa
Mngeresa,ndiye aliyeeleza jambo hilo huku akishangiliwa na wananchi
akimtaka mbunge huyo kumpeleka Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Evarist
Ndikilo,ili atatue kero hiyo kwani Njwayo ameshindwa.
‘’Uuzwaji huu ulifanywa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumbi C ambaye pia
ni Diwani wa Kata ya Chumbi ,Salum Mtimbuko (CCM) na alipata Baraka
kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji,Juma Njwayo,ambaye wananchi
walimueleza suala hilo kabla lakini hakulifanyia kazi na kuwataka waache
majungu’’alisema
Alisema
viongozi hao wamewaudhi wananchi kwa kuuza ardhi kwa muwekezaji ambaye
wanamjua wenyewe na kwamba ukifanyika uchaguzi wakati wowote kabla
masuala hayo hayajataftiwa ufumbuzi CCM itapoteza nafasi hivyo kumuomba
Mbunge huyo kufanya jitihada za kuwaleta viongozi wa mkoa,Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Akizungumzia
suala hilo Mchengerwa alilaani kitendo cha viongozi hao kutaka
kukwamisha maendeleo ya viwanda jimboni hapo kwani alishazungumza na
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage,kuhusu ujenzi wa
kiwanda cha sukari katika eneo hilo ambalo kwa sasa wananchi wamesema
halipo.
‘’Jamani
huku ni kurudishana nyuma na kutotambua juhudi za serikali na
tunaowatetea haiwezekani viongozi wahusike kuuza ardhi ya
kiwanda,wananchi tusikubali,sheria inaruhusu kuongea upya na muwekezaji
huyo ili atuachie ardhi yetu au aongeze fedha tukatafute eneo
linguine,kuuza shilingi 10,000 ekari moja ni aibu’’
Akijibu
tuhuma hizo diwani huyo alisema’’Nyie mnanionea wivu,wengine
nimewasadia sana kuwalisha na familia zenu alafu mnanisema hapa,au
kwasababu mnaniona naishi vizuri na wake zangu wawili na nina nyumba na
magari? Pumbavu’’
Hata
hivyo majibu ya diwani hiyo yalizua tafrani kwa wananchi kumzoea na
kumtaka Mchengerwa arudi kwa mara nyingine na Mkuu wa Mkoa wa
Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,Ili aweze kutatua kero zilizopo kwani
viongozi wanauza maeneo kiholela na wanaposhitaki wa Mkuu wa Wilaya
anakuwa upande wa wauzaji ardhi.
Mchengerwa
aliwaleza wananchi hao kwamba ameshawasiliana na Mhandisi Ndikilo
,kuahidi kufanya ziara katika maeneo hayo Desemba 5 mwaka huu .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni