RC SINGIDA AWAAGA VIJANA WAHADZABE 43 WANAOENDA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa 
Singida Bw. Buhacha Baltazar Kichinda ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi 
sehemu ya utawala na rasilimali watu akiwaaga Vijana 43 wanaojiunga na 
kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa 
miaka ya miwili. Bw. Kichinda amesema wakiwa jeshini watafundishwa 
uzalendo, ukakamavu, stadi za jamii na nidhamu, amewaasa wazazi 
kuwapeleka shule wanafunzi na kupokea fursa kama za jeshi.
Vijana 43 wa kihadzabe wakipanda 
mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 
kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara 
baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya 
kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda 
ya porini, asali na mizizi.
Mmoja wa kijana wa kihadzabe 
Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza vijana wenzake 
wanawinda na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na jeshi ili aweze 
kuisaidia familia yake lakini pia aweze kulitumikia taifa.
Vijana 43 wa kihadzabe wakipunga 
mikono kuonyesha utayari wa kujiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi 
cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya 
kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe 
huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, 
asali na mizizi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni