Jumamosi, 17 Desemba 2016

MAYODA yaomba Serikali kushirikiana na Sekta binafsi

MWENYEKITI Mtendaji wa Mayoda Economic Development Group, Agustino Matefu, ameishauri serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza viwanda vidogovidogo na kuongeza thamani ya bidhaa nch
 aini
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Mayoda Economic Development Group, Augustino Matefu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutoa wito kwa serikali kuunga mkono sekta binafsi ili kukuza uchumi kupitia Viwanda vidogovidogo kupitia wajisiriamali mbalimbali. Katikati ni Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Iddi Majuto na Mratibu wa taasisi hiyo Cleopas John. (Picha na Raymond Urio)

Matefua alitoa ushauri huo jijini Dar es Salaam jana, alipozunguzma na waandishi wa habari juu ya fursa mbalimbali zilizopo nchni.
“Ukiimarisha viowanda vidogovidogo ndio mwanzo wa kukua kwa uchuni nchini, hivyo kuwaunganisha watu katika vikundi na kurasimisha shughuli zao”. Alisema Agustino.
Alisema Mayoda imekuwa ikiwakutanisha wajasiriamali mbalimbali wakiwemo wavuvi, wakulima, wafugaji, mama ntilie na bodaboda na kuwafundisha fursa zilizopo nchini ikiwemo kuwasaidia kupata mikopo mbalimbali.

Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Mayoda Economic Development Group, Augustino Matefu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutoa wito kwa serikali kuunga mkono sekta binafsi ili kukuza uchumi kupitia Viwanda vidogovidogo kupitia wajisiriamali mbalimbali. Katikati ni Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Iddi Majuto na Mratibu wa taasisi hiyo Cleopas John. (Picha na Raymond Urio)

“Mayoda inatoa elimu na kuunda vikundi vyenye wataalamu  mbalimbali ili kuwasajili na kupata uwezashaji ambao huvisaidia baadae kuwa viwanda vidogo vidogo, “ alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni