AZAM SPONSOR FEDERATION CUP KUENDELEA KESHO DES. 3, 2016
RAUNDI ya Tatu ya michuano ya
Kombe la Shirikisho la Azam 2016 (Azam Sports Federation Cup 2016)
inatarajiwa kuendelea kesho Desemba 3, 2016 kwa michezo minne
itakayokutanisha timu nane zilizofanya vema raundi ya kwanza na pili.
Michezo ya kesho ambayo itakuwa mubashara (live), kupitia chaneli mbalimbali za Kituo cha Televisheni cha Azam ‘Azam Tv’ itakuwa ni kati ya Mtwivila ya Iringa na Jangwani ya Rukwa mchezo unaotarajiwa kufanyika mkoani Iringa wakati Stand ya Bagamoyo itacheza na Mbuga ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Stand Misuna ya Singida
inatarajiwa kuwa wenyeji wa Kabela City ya Shinyanga kwenye Uwanja wa
Namfua mjini Singida wakati Mulusagamba ya Kagera na Baruti ya mkoani
Mara zitachuana kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera katika
mfululizo wa mechi hizo.
Mechi hizo zitatoa timu nne bora kutoka mabingwa wa Mkoa na hivyo kuungana na timu 24 za Ligi Daraja la Pili kwa michezo ya hatua ya raundi ya nne na tano kutafuta timu nane bora zitakazosonga mbele kukutana na timu za Daraja la Kwanza.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni