Jumamosi, 17 Desemba 2016

PROF. MBARAWA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA

prof
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kisorya Wilayani Bunda, mkoani Mara wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani hapo.
prof-1                                            
Mbunge wa Mwibara Mhe. Kange Rugora (wa pili kushoto), akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), katika ziara yake mkoani Mara wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya kilichopo Wilaya ya Bunda.
prof-2
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Eng. Fredinand Mishamo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea na kukagua kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani hapo.
prof-3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akishuka kutoka katika kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani Bunda, wakati alipotembelea na kukagua kivuko hicho.
prof-4
Muonekano wa kivuko cha MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Rugenzi Ukerewe na Kisorya wilayani Bunda.
prof-5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kivuko cha MV Mara kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Mugara na Kuruge wilayani Bunda, wakati alipotembelea na kukagua kivuko hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwl. Lydia Bupilipili.

kero
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisikiliza kero kutoka kwa mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Iramba, Wilaya ya Bunda, mara baada ya kukagua kivuko cha MV Mara na kuongea na wananchi hao.
athari
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiangalia athari za miundombinu ya barabara kwenye Daraja la Burendabufwe lilibomoka kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni katika barabara ya Kibara-Iramba wilayani Bunda.
prof-6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akicheza nyimbo za asili za kabila la wakerewe, wilaya ya Bunda kabla ya kuongea na wakazi wa kijiji cha Iramba, mkoani Mara.
prof-7

Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mhe. Kange Lugora (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwibara.
………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewaagiza Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wa Halmashauri kote  nchini 
kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia kwa ukaribu utekelezaji 
wa miradi mbalimbali  inayotekelezwa kwa kutumia Mfuko wa Barabara katika maeneo yao.
Akizungumza Wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya kupokea taarifa ya hali ya miundombinu Wilayani hapo, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa hatua hiyo pia itasaidia kudhibiti upotevu wa fedha za wananchi pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya wote na Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara ambazo ni fedha za wananchi”, ameagiza Prof. Mbarawa.
Aidha, amemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Bunda kuwa Serikali itaendea kufanya kila linalowezekana kuimarisha miundombinu kwa maendeleo ya watanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl.Lydia Bupilipili, amesema kuwa wilaya hiyo imejiwekea utaratibu  wa kufuatilia miradi hiyo lakini pia inawaelimisha watendaji kata na vijiji kuhusiana na sheria ya barabara.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea Kivuko cha Mv Mara na Mv Ujenzi na kuahidi kuboresha utoaji wa huduma katika vivuko hivyo ikiwemo ujenzi wa jengo la abiria katika kijiji cha Iramba na Kisorya.
Amewasisitiza kudhibiti mapato yatokanayo na vivuko hivyo ili kuweza kuongeza ufanisi na utendaji wa vivuko hivyo.
Naye, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoani Mara amemhakikishia Waziri huyo kufunga mifumo ya kielektroniki ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa ametembelea barabara ya Busambala – Kisorya (KM 120), na kutoridhishwa na hatua ya ujenzi wake, hivyo kutoa miezi sita kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Roads Works anayejenga barabara hiyo kukamilisha ujenzi wake.
Prof. Mbarawa ameanza ziara yake ya siku mbili mkoani Mara ambapo anatarajia kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kitengo cha Mawasiliano Serikalini

ZIARA YA MAJALIWA HALMASHAURI YA ARUSHA

ngoma
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
piga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ziduka
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
twisha
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaaa
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao   walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama  ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha  Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaa-2222
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu  wilayani Arusha ambao wlijipanga  kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DK. MAGUFULI AMPA KAZI PROFESA YUNUS MGAYA KUWA MKURUGENZI WA (NIMR), ALIAHIDI KUMPA KAZI NYINGINE BAADA YA KUTUMBULIWA (TCU)

nimr

NAPE AFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI WILAYANI KARATU.

ria1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu (Karatu Sports Festival).
ria2
Wanariadha wanaoshiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu wakijandaa kuanza kukimbia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Disemba 17/2016.
ria3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimkia na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
ria4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimkia na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
ria5

KAMPUNI YA NAMAINGO KUGAWA SUNGURA 600 KWA WAJASIRIAMALI DAR

sugu
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim (kulia0 na Meneja Mradi wa Sungura wa kampuni hiyo, Amos Misinde wakionesha kwa wanahabari, Dar es Salaam jana,  baadhi ya sungura 600 zitakazogawiwa leo kwa Wajasiriamali 2000. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


Na Richard mwaikenda
KAMPUNI ya Namaingo, kugawa sungura 600 kwa Wajasiriamali 2000 Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa nchini.


Mpango huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim katika mkutano na waandishi wa habari eneo la mradi huo wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam jana.


Alisema kuwa walengwa watakaonufaika na mradi huo, ni Wakulima  3000 waliojiunga katika vikundi vya ushirika 30 kutoka katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kila kikundi kina wakulima 50.


Biubwa alisema  kwa kuanzia ni vikundi 20 vya ushirika vyenye Wajasiriamali 2000 ndiyo watakaogawiwa sungura leo na wengine 1000 watafuata baada ya sungura hao kuzaliana. Kila kikundi kipatiwa sungura wazazi 27 na dume watatu.


“Hadi sasa tuna vikundi  30 vya ushirika, tutaanza mradi na vikundi 20 vitakavyopatiwa sungura kama mbegu ya kuzalisha kwa ajili ya kupatiwa vikundi vingine 10 vilivyobakia,” alisema Biubwa. 


Alisema kuwa ndani ya miezi mitano sungura wazazi 540 watakuwa wamezaa mara tatu, hivyo kuwa na watoto 9,720. Jumla hiyo inatokana na kila sungura mzazi mmoja kuzaa watoto 6.


Alisema mpango utakaofuata ni kila mwanachama kugawiwa sungura 8 kwa ajili ya kuendeleza ufugaji na kupata kipato kitakachosaidia katika maisha yao.


Akielezea faida ya ufugaji wa sungura, Meneja wa Mradi huo, Amos  Misinde alisema kuwa nyama ya sungura inahitajika sana na kwamba hadi sasa zinahitajika tani 5 za nyama hiyo kwa wiki. Sungura wakifugwa kwa uangalizi mzuri mmoja anaweza kufikisha uzito wa kilo 8 ambapo kilo moja ya nyama ni sh. 8,500.


Wanahabari walipata wasaa wa kutembezwa kwenye mabanda kuwaona sungura hao walioingizwa nchini wiki hii kutoka Kenya.
Sungura hao wapo chini ya uangalizi wa watalaamu kutoka Rabbit Republic ya Kenya, Suma JKT na Namaingo Business Agency pamona na watalaam wengine kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).




 Biubwa akimwingiza mmoja wa  sungura kwenye banda eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam
 Biubwa akifafanua jambo mbele ya wanahabari alipokuwa akielezea kuhusu mradi huo
 Wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati Biubwa akizungumza nao
 Meneja Mradi wa Sungura wa Kampuni ya Namaingo, Amos Misinde akionesha sungura waliokwenye mabanda tayari kuwagawia wajasiriamali leo
 Mabanda yenye sungura
 Sungura wanaosubiri kuwekwa kwenye mabanda
 Sungura akila majani
 Meneja Masidizi wa Mradi wa Sungura, Denis Rugezia akiwa na sungura tayari kumpanga kwenye moja ya mabanda
 Mmoja wa wafanyakazi akiwapeleka sungura kwenye mabanda. Sungura hao wamewasili kutoka Kenya.

 Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), akiwanesha wanahabari sungura dume
 Mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, Richard Mwaikenda akiangalia mabanda yenye sungura
 Mmiliki wa Bongo weekend blog Khadija Kalili akikagua mabanda hayo
 Mmoja wa wanufaika wa mradi huo akiwa kwenye mabanda hayo
Makao Makuu ya Mradi wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam.

WASIOENDELEZA MASHAMBA ARUMERU KUNYANG’ANYWA-MAJALIWA

pikaaaa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itawanyang’anya ardhi wamiliki wote wa mashamba makubwa wilayani Arumeru ambao hawajayaendeleza kwa sababu wamekiuka mkataba wa umiliki.
Amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi atakuja mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya mapitio ya mashamba yote makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyarudishwa Serikalini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Desemba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru na wananchi wa kijiji Bwawani na kitongoji cha Mapinu katika kata ya Nduruma akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.
“Tufanya mapitio ya kila shamba ili kujua linamilikiwa na nani na alipewa lini na tangu alipokabidhiwa amefanya nini. Shamba lisiloendelezwa litarudisha kwa wananchi. Kama mtu ameshindwa kupata mtaji kwa muda wa miaka 10 atapata leo,” amesema.
Amesema Serikali haiko tayari kuona wananchi wakinyanyaswa kwa kukosa ardhi ya kilimo kwa sababu ya watu wachache kumiliki maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza..
“Ninataarifa kwamba hapa Arumeru kuna baadhi ya wawekezaji wanamiliki mashamba makubwa na hawajayaendeleza. Wengine wanakodisha kwa wananchi ili kujipatia fedha kinyume na mikataba yao ya umiliki. Hatutawavumilia,” amesema.
Amesema wilaya ya Arumeru inaongoza kwa migogoro ya ardhi na maeneo mengi yametwaliwa na mtu mmoja mmoja na baadhi yao wamekuwa wakilitumia vibaya Jeshi la Polisi kwa kuwanyanyasa wananchi wanaokatiza au kulima kwenye maeneo hayo.
“Kuanzia leo marufuku Jeshi la Polisi kutumiwa na mtu binafsi kuwanyanyasa wananchi. Mtafanya hivyo kama kuna uvunjifu wa amani na si vinginevyo,” amesema.
Awali, akisoma taarifa ya wilaya mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw. Alexander Mnyeti  alimweleza Waziri Mkuu kwamba wilaya hiyo ina mashamba makubwa yanayomilikiwa na wawekezaji ambayo hayajaendelezwa.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kitendo cha kutoyaendeleza mashamba hanayo kisababisha wananchi kuyavamia hali inayochangia kushamiri kwa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
Amesema tayari ofisi yake imefanya uhakiki wa mashamba hayo na kumuomba Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli kufuta hati za mashamba 12 ambayo hayajaendelezwa kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali imepeleka sh. bilioni 800 katika halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akizindua nyumba ya walimu na vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari ya Orjolo, hatua ambayo inalenga kuboresha mazingira ya kufanyiakazi na kupunguza changamoto ya makazi kwa walimu.
Amesema changamoto ya makazi imekuwa ikiwakabili walimu kwa mrefu hivyo  Serikali imeamua kujenga nyumba za gharama nafuu ambazo zinawezesha familia sita kuishi pamoja.
Pia amewataka wazazi kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule na kuhakikisha wanafuatilia miendendo ya elimu kwa watoto wao.
“Tumeondoa ada na michango yote iliyokuwa inawakera na kusababisha mshindwe         kuwapeleka watoto shule. Jukumu lenu kwa sasa ni kufuatilia mienendo ya watoto wenu hadi kwa walimu ili kuhakikisha wanaingia darasani na wanasoma,” amesema.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk, Wilson  Mahera alisema mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari ya awamu ya pili (SARPCCO II) umewezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 4,vyoo 20 pamoja na vyumba vya madarasa 6 vyenye jumla la Sh. milioni  289.52.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, DESEMBA 17, 2016.