KIGOMA MJINI WAMPONGEZA LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YAO YA ARDHI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi anaendelea na ziara ya siku tatu 
katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi Baraza la Ardhi na Nyumba 
la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa 
Kigoma. Wananchi hao wamempongeza Mhe. Waziri kwa hatua anazozichukua 
katika kumaliza migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na 
Nyumba ambalo jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa 
nchini.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akifungua Baraza la Ardhi na 
Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto 
Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Jenerali Emanuel 
Maganga.
 Jingo jipya la Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
 Samani mpya za Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na 
Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akiongea na wananchi wa Kigoma 
Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi.
Wananchi wa Kigoma Mjini 
wakiwasilisha malalamiko yao ya migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, 
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi ili yaweze kutatuliwa.
Wananchi wa Kigoma mjini wakimsikiliza Waziri wa Ardhi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni