MALINZI AOMBOLEZA VIFO VYA WACHEZAJI WA CHAPECOENSE YA BRAZIL.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu 
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa 
Shirikisho la Mpira Brazil (CBF), kutokana na vifo vya wachezaji wa timu
 ya soka Chapecoense Real ya Brazil.
Rais wa TFF Malinzi, katika salamu za 
rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil (CBF), Lucca 
Victorelli  amesema ajali hiyo iliyoua watu wengi ni tukio la 
kusikitisha kwenye familia ya soka duniani na limetokea katika kipindi 
kigumu.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni