Jumatano, 30 Novemba 2016

Serikali ya kabidhi Bendera kwa Timu ya Taifa ya Kuogelea kwenda kushiriki mashindano nchini Canada



Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam
30/11/2016.
mpira
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya bendera kwa timu ya taifa ya kuongelea inayotarajia kwenda nchini Canada  leo jijini Dar es Salaam .
mpira-1
Meneja Mauzo kutoka Kampuni ya errea iliyopo Italy Bw. Affri Minidji  Droctovee  akizungumza na waaandishi  wa Habari (hawako pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu dhamira ya kampuni ya errea kuisaidia timu ya taifa ya kuogelea inayokwenda katika mashindano nchini Canada mapema mwezi Desemba mwaka huu. Kulia ni Balozi wa Italy nchini Mhe. Roberto Mengoni.
mpira-2
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa kwanza kulia) na Balozi wa Italy nchini Mhe. Roberto Mengoni (wapili kulia) wakimkabidhi nahodha wa timu ya taifa ya kuogelea Bw. Hilal Hemed Hilal (wapili kushoto) jezi za wanamichezo wa timu hiyo leo jijini Dar es Salaam, zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya errea kutoka Italia kwa ajili ya kudhamini timu hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Mauzo kutoka Kampuni ya  errea Italy Bw. Affri Minidji  Droctovee
mpira-3
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya taifa ya kuogelea Bw. Hilal Hemed Hilal (kushoto) leo jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa akiaga timu hiyo inayokwenda nchini Canada kushiriki mashindano yanayotarajia kuanza mapema mwezi Desemba mwaka Taifa huu.
mpira-4
Kocha wa Timu ya Taifa ya Kuogelea inayotarajia kwenda nchini Canada katika mashindano ya kuogelea mapema mwezi Desemba mwaka huu Bw. John Belela (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya wachezaji kuelekea mashindano hayo katika hafla ya kukabidhiwa bendera na serikali. Kutoka kulia ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura na kushoto ni Balozi wa Italy nchini Mhe. Roberto Mengoni.
mpira-5
Mmoja wa wanamichezo wa timu ya taifa ya kuogelea watakaoshiriki katika mashindano ya kuogelea nchini Canada mapema Desema mwaka huu  Bw. Dennis Mhini akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi yake na kutoa ahadi ya kurudi na ushindi pamoja na kuliletea taifa heshima Duniani.
*********************************MWISHO*******************

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni