Jumatano, 30 Novemba 2016

SIMBA YASHUSHA KIPA MPYA TOKA MEDEAMA FC YA GHANA.


agy

Baada ya taarifa kuenea kuwa Simba inataka kusajili golikipa toka Ghana hatimaye ametua rasmi kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Kocha Joseph Omog.

Kipa huyu Daniel Agyei alikuwa anakitumikia kikosi cha Medeama FC ambayo ilicheza na Yanga katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, kipa huyo alipokelewa na Mratibu wa Simba, Abbas Ally na atakuwa akitoa changamoto kwa golikipa wa sasa Vicent Agban ambaye alikosa mshindani kutokana na uwezo wa Manyika Peter na Denis Richard kuonekana kuwa hawakuwa na kiwango cha juu pamoja na kukosa uzoefu katika mikikimiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni