STAR MEDIA (TANZANIA) LIMITED yazindua televisheni mpya yenye king'amuzi ndani yake...
A ELIZABETH VICENT, Dar
KAMPUNI ya StarTimes Tanzania jana ilizindua televisheni
mpya ya kidigitali ambayo ina king'amuzi ndani na itawezesha wateja wake
kuangalia chaneli mbalimbali bila usumbufu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugenzi Mkuu wa Star
Times Tanzania, Lanfang Liao alisema kuwa kama kampuni imeamua kutoa
television hizo za kisasa kulingana na ukuaji wa teknlojia ambapo wateja
wataweza kuona vipindi vinavyoendana na wakati.
"Tutahakikisha tunawapa wateja wetu vipindi vyenye ubora
huku wakifurahia Ulimwengu wa kidigitali kwa bei nafuu, lakini tunafahu
kuwa msimu huu ni wa sikukuu hivyo ni lazima wateja wapate kitu tofauti
kitakachoafurahisha" alisema Liao
Akizungumzia ubora wa Televisheni hizo alisema kuwa ni
miongoni mwa televisheni ambazo zimeunganishwa na king'amuzi moja kwa
moja huku zikiwa na matumizi madogo ya umeme tofauti na televisheni za
kawaida ambazo zenyewe hutumia WAT200 kwa saa.
Aidha Liao alisema kuwa televisheni hizo zina chaneli zaidi
ya mia moja ambapo zina uwezo wa kuonyesha vipindi mbalimbali vyenye
kuelimisha na kuburudisha jamii.
"Televisheni hizo zina ukubwa tofauti ambapo zinapatikana
kwa inchi 40,32, pamoja na inchi24 huku zikiwa na vifurushi vya mwezi
mmoja bure" alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu kutoka Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Maria Sasabo alisema kama serikali
itaendelea kuchunguza kwa umakini bidhaa zinazotumia teknolojia ya
kidigitali ili kupima uwezo wa bidhaa hizo nchini.
"Suala la Teknlolojia na mawasiliano linachukua nafasi
kubwa katika taifa letu, hivyo kwa kitu chochote kinachozinduliwa ni
lazima tupime ubora wake na hapa tunashukuru Star times kwa kutupatia
serikali televisheni moja ambayo tutaenda kuipima kama wizara husika"
alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni