MAKINDA:AWATAKA WANAWAKE WASIKATE TAMAA BALI WAPIGANIE HAKI ZAO
Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Anne Makinda aliyekuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la kwanza la kitaifa la haki za Wanawake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la msaada wa kisheria Legal Services Facility (LSF).
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za binadamu Dr.Hellen Kijo Bisimba akiongea katika kongamano hilo.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Wanawake wa kitanzania wametakiwa kupigania haki zao bila kujali vikwazo wanavyokutana navyo katika mchakato wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia katika kada zote, huku wakisaidiana na kujiamini katika kufikia lengo lao la kuhakikisha haki za wanawake zinasimamiwa.
Hayo yamesemwa na spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe, Anne Makinda, jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la kwanza la kitaifa la haki za wanawake.
Mhe, Makinda alisema kuwa wanawake waache kuwa nyuma badala yake wasimame kuzipigania haki zao na kuhakikisha kuwa malengo ya kumkomboa mwanamke yanafikiwa bila kukatishwa tamaa na vikwazo vilivyopo ikiwemo mfumo dume unao zaa unyanyasaji wa kijinsia.
“Bila kusimama sisi wenyewe na kuzipigania haki zetu, hakuna anaeweza kutusaidia, hata mimi nisingesimama mwenyewe nisingeweza kufikia nafasi nilizozifikia katika maisha yangu” Alisema mhe, Makinda.
Mhe, Makinda pia aliitaka serikali kuweka mikakati ya namna ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na kutetea haki za wanawake nchini badala ya kutegemea wahisani pekee kwakuwa wao hufanya hivyo kwa kipindi maalum na baada ya hapo mashirika hayo hubaki bila msaada.
Kongamano hilo limeandaliwa na mfumo wa msaada wa kisheria (LSF) na kushirikisha wadau mbalimbali wa kutetea haki za wanawake nchini na kauli mbiu katika kongamano hilo ni “Jitambue, Jiamini,Simamia haki yako”
Awali akizungumza kwemye kongamano hilo, afisa mtendaji mkuu wa LSF, Kess Greonerndijk, alisema kuwa wameamua kusaidia mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na kusimamia haki zao kwakuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa kufanya hivyo kutokana na matukio mengi ya kikatili yanayo ripotiwa kufanywa dhidi ya wanawake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni