Jumatano, 30 Novemba 2016

KIGOMA MJINI WAMPONGEZA LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YAO YA ARDHI


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi anaendelea na ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Kigoma. Wananchi hao wamempongeza Mhe. Waziri kwa hatua anazozichukua katika kumaliza migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na Nyumba ambalo jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa nchini.zit1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akifungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
zit2
Jingo jipya la Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
zit3
Samani mpya za Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
zit4
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akiongea na wananchi wa Kigoma Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi.
zit6 zit7
Wananchi wa Kigoma Mjini wakiwasilisha malalamiko yao ya migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi ili yaweze kutatuliwa.
zit9
Wananchi wa Kigoma mjini wakimsikiliza Waziri wa Ardhi.

MD KAYOMBO AFANIKISHA MRADI SHULE YA MATOSA

kayombo
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amepongezwa
na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Matosa iliyopo Kata
ya Goba , Manispaa ya Ubungo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa
utekelezaji wa mradi wa SEDP II.

Mradi huo unaohusisha ujenzi wa vyumba viwili vya darasa, nyumba za
walimu, kisima cha maji, tanki la kuhifadhia maji pamoja na vyoo upo
katika hatua nzuri ya kukamailika kutokana na juhudi pamoja na utendaji
kazi uliotukuka wa Mkurugenzi Kayombo akishirikiana na watumishi wa
Manispaa hiyo.
Akizungumza na mtandao wetu mwalimu Mkuu wa shule
hiyo alisema amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo za kuleta maendeleo kwa wananchi na kwenda sambamba na
kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
“Napenda
kutoa shukrani Kwa Serikali kwa kuuleta mradi wa SEDP II katika shule
yetu, pia napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa juhudi zake anazozifanya mpaka mradi
umefika hatua hii, kwa kweli ametusaidia sana, mungu ambariki”, alisema
Mwalimu mkuu.
Wakati huo huo wanafunzi wanaosoma katika shule
hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kayombo kwa kazi nzuri aliyofanya mpaka
kuweza kufanikisha kupatikana kwa maji pamoja na madarasa, vyoo, tanki
la maji na nyumba za walimu.

MWILI WA RPC SINGIDA KUAGWA LEO MUHIMBILI


kakamba
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
             WIZARA YA MAMBO YA NDANI
                JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                               Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                             Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                          S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                      DAR ES SALAAM.
                                                                                                                                       
30 /11/2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

KUAGWA KWA MWILI WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA.

Mnajulishwa kuwa mwili wa Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, aliyefariki dunia Alfajiri ya Tarehe 30/11/2016 utaagwa leo tarehe 30/11/2016 Saa 11: 00 (Kumi na moja kamili Jioni) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na baadaye utasafirishwa kwenda Mpanda  Mkoani Katavi kwa ajili ya Mazishi.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi

MALINZI AOMBOLEZA VIFO VYA WACHEZAJI WA CHAPECOENSE YA BRAZIL.


malinziiiiiiiii
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira Brazil (CBF), kutokana na vifo vya wachezaji wa timu ya soka Chapecoense Real ya Brazil.
Rais wa TFF Malinzi, katika salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil (CBF), Lucca Victorelli  amesema ajali hiyo iliyoua watu wengi ni tukio la kusikitisha kwenye familia ya soka duniani na limetokea katika kipindi kigumu.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA YAFUTWA


indexMaadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani, ambayo kitaifa yalitarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam,Desemba 3, mwaka huu yameahirishwa na badala yake kila mkoa utaadhimisha kivyake.
Akitoa tamko la kuharishwa kwa maadhimisho hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema maadhimisho hayo yalilenga kila halmashauri isafirishe wanachama wa vyama vya watu wenye ulemavu ili washiriki maadhimisho hayo jijini humo.
Amesema kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa wakuu wa mikoa kuwa badala ya maadhimisho hayo ya kitaifa kukusanya walemavu wote kwenye mikoa kwenda Dar es salaam yafanyike kwenye mikoa yao.

SIMBA YASHUSHA KIPA MPYA TOKA MEDEAMA FC YA GHANA.


agy

Baada ya taarifa kuenea kuwa Simba inataka kusajili golikipa toka Ghana hatimaye ametua rasmi kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Kocha Joseph Omog.

Kipa huyu Daniel Agyei alikuwa anakitumikia kikosi cha Medeama FC ambayo ilicheza na Yanga katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, kipa huyo alipokelewa na Mratibu wa Simba, Abbas Ally na atakuwa akitoa changamoto kwa golikipa wa sasa Vicent Agban ambaye alikosa mshindani kutokana na uwezo wa Manyika Peter na Denis Richard kuonekana kuwa hawakuwa na kiwango cha juu pamoja na kukosa uzoefu katika mikikimiki.

MEYA WA JIJI LA ARUSHA AZINDUA KAMPUNI YA MASOKO YA KISMATY ADVERT MEDIA

 Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company Ltd, Bi. Mary Emmanuel Mollel akizungumza Machache katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd Mary Emmanuel ,akisalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Wa kwanza kulia ni Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro , mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Co. Ltd, Bi. Mary Emmanuel ,na Mratibu wa shughuli hiyo Bi. Dotto Kimaro katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini
Arusha, Novemba 25 ,2016.
Mchekeshaji ‘Steve Nyerere’ nae hakubakia nyuma alikuwepo akifanya yake katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.






Watatu kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Calist Lazaro ,Naibu meya Bi. Viola Lazaro ,Diwani wa kata ya Themi Kinabo na Diwani wa kata ya Levolosi Ephata Nanyaro katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Wa pili Kutoka Kushoto ni Meneja wa Venus Hotel Mr. Prashant akiongozana na mkewe na rafiki yao Mr. Dibin wakiwa katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.

MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA



zuku
 Meneja Mkuu wa Zuku
Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi akiongea na waandishi
wa habari juu ya huduma mpya ya
TV ya nishati ya jua ambayo ina
channel za
Zuku Tv
 katikati ni
Afisa masoko wa Mobisol
Sjors Martens akiwa na wafanyakazi wa mobiso l katika uzinduzi huo hii
leo jijini Arusha
 mmoja wa mmteja wa mobisol
ambaye akutaka kutaja jina lake akiongea wakati wa uzinduzia ambapo
aliisifia kampuni ya mobisol nakusema ni mtetezi wa wananchi wanaoishi
vijijini ambapo umeme haujafika
 Meneja wa zuku Tanzania wa
kwanza kushoto akibadilishana mawazo na wa kwanza kulia ni afisa
usiano wa Zuku  dada Yasta pamoja na  mwakilishi wa
zuku  Jack Karanja katika uzinduzi
 wafanyakazi wa zuku wakifurahia
mara baada ya uzinduzi
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;}

 

 Na Woinde
Shizza,Arusha
 KAMPUNI
inayoongoza kwa utowaji wa huduma za
nishati ya jua majumbani ,Mobisol na Kampuni ya Zuku Tv inayotoa burudani za
satellite wameungana  pamoja kwa ajili
kuwanufaisha watanzania wasiounganishwa na nishati ya
umeme. 
Kwa pamoja kampuni
hizi zimezindua kwa mara ya kwanza TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za
Zuku Tv  huduma inayowalenga wale ambao
hawajafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.




Huduma hii huunganisha
mfumo  wa nishati jua, televisheni ya hadi inchi 32
ya nishati jua, ungo wa satellite, na huduma ya ya kifurushi cha Zuku Smart
Plus chenye chanelli 47 and 18 za redio. Mobisol wanalenga
kutoa huduma hii kwa watanzania ambao hawajafikiwa
na huduma ya nishati ya umeme, kwa  kutoa
nashati safi na ya kuaminika kwa bei nafuu popote ulipo katika mfumo moja
mkamilifu.




Mobisol inatoa vifurushi
mbalimbali vya nishati ya jua ya
majumbani, vilivyo na uwezo wa kutoa nguvu ya umeme hadi
200W,  unaotosha matumizi ya kaya nzima. Kila
kifurushi kintaota paneli ya PV, betri ya nishati ya jua, taa nne za mwanga
mkali,TV kubwa ya kioo cha  bapa, tochi,
chagi ya simu na redio ambayo unaweza kuichagi. Vifaa hivi vinapatikana na
waranti, huduma ya kufungiwa bure, huduma ya wateja na huduma ya marekebisho
kwa miaka 3.  Pia,
Kwa kuongezaTsh 8,999 kwamwezikwakifurushi,
watejawatawezakupatahudumazaZuku
TV kwamudawamasaasabakwasiku .




Akizungumza katika
uzinduzi  huo   Afisa masoko wa Mobisol
Sjors Martens alisema kuwa wao wanania ya kuleta maisha mazuri kwa wateja
wao nchini Tanzania. 
Alisema Huduma yao  ya
kifurushi cha televisheni ya satellite
kitawezesha wateja  kufurahia habari , michezo, burudani na maudhui ya
elimu wakati wowote hata wakiwa wanaishi
mjini au vijijini.




Kwa upande wake Meneja Mkuu
wa Zuku Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi alisema
ubunifu wa huduma
hii itatuwezesha kufikia zaidi ya watanzania million 8 ambao hawajawa na
nishati ya umeme wa grid ya Taifa na kutuwezesha kuchangia kwa asilimia kubwa
ongezeko la televesheni
nchini. 
  “Hii ni
fursa ya kipekee na ya kuleta hamasa  kwa
wateja wa Mobisol kuwa na uwanja mpana zaidi
wa kuchagua na kufurahia zaidi ya chaneli 40 za Zuku TV inayotambulika
kama huduma bora ya bei nafuu inayotoa burudani kwa
familia kwa kuhamasisha  maudhui ya
kinyumbani zaidi,” alisema Zuberi.




Aliongeza kuwa Ingawa
asilimia 70 ya watanzania hawajafikiwa na huduma ya
nishati ya umeme na asilimia kubwa ya watanzania bado hawana Televisheni,
Mobisol na Zuku wametumia fursa hii na kuungana pamoja kwa ajili ya kutoa
huduma ya umeme wa jua na kutoa burudani ya TV Satellite yenye ubora wa
kimataifa




 Aidha alisema kuwa
Huduma hii ya PayTV  iliozinduliwa mkoani hapa itapatikana katika
mikoa ambayo
Mobisol inatoa huduma ambapo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani,
Singida, Tabora, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Simiyu, Mbeya,
Songwe na Njombe – na baadaye kote nchini mwaka
ujao




Alibainisha kuwa Kupitia Zuku
TV, watanzania wanaweza kufurahia idadi ya
channel  za kusisimua ikiwa ni pamoja na
channel  za nyumbani  FTA,
channel
za kimataifa na channel za  Zuku
asili; Zuku Sports, hivi karibuni ilizindua tena
Zuku Swahili, Zuku Kids, Zuku Life Glam na
Zuku Nolly.




Alisema kuwa Bei ya kifurishi
cha Zuku smart pack kitakuwa kikiongezwa
kwa awamu katika mfumo nishati ya
jua  ya Mobisol, ambayo wateja hulipa
kupitia  simu  kwa kipindi cha
miaka mitatu.
Alifafanua kuwa  Baada
ya miaka
mitatu, wateja watamili hivyo vifaa  na
kupata ofa ya kuvutia kwa kulipa tena huduma hiyo
mpya

PLAN INTERNATIONAL YAZINDUA MRADI WA KUWAWEZESHA VIJANA NA WATOTO KUPITIA MICHEZO.


plav1
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani, Wanchoko Chinchibera akiongea na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo uliozinduliwa leo wilayani humo.Mradi huo unaratibiwa na Shirika la Plan International.
plav2
Meneja Miradi wa Shirika la Plan International, Grace Semwaiko akielezea kuhusu malengo ya mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo uliozinduliwa leo wilayani Kisarawe.Mradi huo unaratibiwa na Shirika la Plan International.
plsv3
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani, Wanchoko Chinchibera akikagua timu ya mpira ya watoto wakati wa mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo uliozinduliwa leo wilayani humo.Mradi huo unaratibiwa na Shirika la Plan International.
…………………………………………………………………
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
 
Shirika la Plan International limezindua Mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo ili kuwajengea uwezo wa kuwa mawakala hai wa mabadiliko chanya katika jamii zinazowazunguka.
 
Mradi huo umezinduliwa leo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo, Wanchoko Chinchibera ambaye ametoa wito kwa watendaji wa Serikali, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha mradi huo unatekelezeka.
 
Chinchibera amesema mradi huo umekuja wakati muafaka kwani watoto na vijana wanakabiliwa na changamoto ya ulinzi, usawa wa kijinsia pamoja na ushirikishwaji mdogo katika michezo hivyo kupitia mradi huo watapata maendeleo mazuri ya kielimu na kimakuzi pamoja na fursa ya kutatua changamoto zao.
 
“Kupitia michezo tunajenga afya, akili, malezi na makuzi ya mtoto lakini pia michezo ni sehemu ambayo watoto wanaweza kupaza sauti zao na kujadili kuhusu haki zao za msingi kwa njia ya nyimbo na mashairi hivyo tunaamini kuwa tukianza kuwashirikisha watoto katika suala zima la michezo tutatengeneza kizazi chenye maendeleo,”alisema Chinchibera.
 
Ameongeza kuwa kupitia michezo, vipaji vingi vitaibuliwa ambavyo vitasaidia katika kutengeneza ajira mbalimbali zitakazowawezesha vijana kujikomboa kiuchumi na kuchangia katika pato la taifa hivyo amewahakikishia wananchi kuwa mradi huo utazaa matunda mazuri.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa Shirika hilo, Grace Semwaiko amesema mradi huo ni sehemu ya mpango mkakati wa tatu wa shirika hilo ambao kwa ujumla unalenga kufikia jumla ya watoto 3,075 na vijana 3,109 katika kuwahakikishia ulinzi na usawa wa kijinsia.
 
“Ni matumaini yetu kuwa mradi huu utatekelezwa vizuri na hatimaye kufikia malengo tuliyojipangia yakiwemo ya kukua kwa uelewa kwa jamii na wadau wote kuhusu usawa wa kijinsia, kuhakikisha vijana na watoto waliowezeshwa wanaleta mabadiliko katika jamii pamoja na kuimarika kwa ulinzi wa watoto katika ngazi ya jamii hadi taifa,” alisema Bi Grace.
 
Alifafanua kuwa mradi huo unawalenga wanafunzi wa Shule za Msingi kuanzia darasa la 4 hadi la 7, wanafunzi wa Shule 6 za Sekondari, walimu, wazazi, viongozi wa jamii na watendaji wa Vijiji, Kata pamoja na Watoto na Vijana ambao hawasomi.
 
Mradi huo utaratibiwa na shirika la Plan International pamoja na shirika la Right to Play na utatekelezwa katika Kata mbili za Kiluvya na Malumbo zilizopo wilayani humo ambapo jumla ya vijiji 10 vitanufaika.
 
Aidha Bi.Grace aliongeza kuwa Mradi huo unatarajiwa kuwa wa miaka miwili na utagharimu jumla ya shilingi 641,468,700 ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2018.
 
Shirika la Plan International la nchini Ujerumani ni miongoni mwa mashirika ya Kimataifa yasiyo ya kiserikali ambayo yameonyesha juhudi kubwa za kuibua miradi mbali mbali katika jamii na kuifadhili katika sekta za Afya,Maendeleo ya jamii,Wanawake,Watoto na Michezo.

Serikali ya kabidhi Bendera kwa Timu ya Taifa ya Kuogelea kwenda kushiriki mashindano nchini Canada



Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam
30/11/2016.
mpira
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya bendera kwa timu ya taifa ya kuongelea inayotarajia kwenda nchini Canada  leo jijini Dar es Salaam .
mpira-1
Meneja Mauzo kutoka Kampuni ya errea iliyopo Italy Bw. Affri Minidji  Droctovee  akizungumza na waaandishi  wa Habari (hawako pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu dhamira ya kampuni ya errea kuisaidia timu ya taifa ya kuogelea inayokwenda katika mashindano nchini Canada mapema mwezi Desemba mwaka huu. Kulia ni Balozi wa Italy nchini Mhe. Roberto Mengoni.
mpira-2
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa kwanza kulia) na Balozi wa Italy nchini Mhe. Roberto Mengoni (wapili kulia) wakimkabidhi nahodha wa timu ya taifa ya kuogelea Bw. Hilal Hemed Hilal (wapili kushoto) jezi za wanamichezo wa timu hiyo leo jijini Dar es Salaam, zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya errea kutoka Italia kwa ajili ya kudhamini timu hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Mauzo kutoka Kampuni ya  errea Italy Bw. Affri Minidji  Droctovee
mpira-3
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya taifa ya kuogelea Bw. Hilal Hemed Hilal (kushoto) leo jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa akiaga timu hiyo inayokwenda nchini Canada kushiriki mashindano yanayotarajia kuanza mapema mwezi Desemba mwaka Taifa huu.
mpira-4
Kocha wa Timu ya Taifa ya Kuogelea inayotarajia kwenda nchini Canada katika mashindano ya kuogelea mapema mwezi Desemba mwaka huu Bw. John Belela (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya wachezaji kuelekea mashindano hayo katika hafla ya kukabidhiwa bendera na serikali. Kutoka kulia ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura na kushoto ni Balozi wa Italy nchini Mhe. Roberto Mengoni.
mpira-5
Mmoja wa wanamichezo wa timu ya taifa ya kuogelea watakaoshiriki katika mashindano ya kuogelea nchini Canada mapema Desema mwaka huu  Bw. Dennis Mhini akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi yake na kutoa ahadi ya kurudi na ushindi pamoja na kuliletea taifa heshima Duniani.
*********************************MWISHO*******************

Jumatatu, 28 Novemba 2016

Wanafunzi Wasichana wametakiwa kuweka bidiii katika masomo ya Sayansi

Mwenyekiti wa Shule ya Sekondari ya Wama Nakayama ambaye pia ni mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi zawadi mgenoi rasmi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya wakati wa Sherehe ya Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Wama Nakayama iliyopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani 26 Novemba, 2016.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
nyami3
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Shule, wageni waalikwa pamoja na Wahitimu wa Kidato cha Nne baada ya kumalizika Sherehe ya Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Wama Nakayama iliyopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani 26 Novemba, 2016.
nyami2
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa Kidato cha Nne wakati wa Sherehe ya Mahafali ya Nne ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Wama Nakayama iliyopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani 26 Novemba, 2016.
…………………………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
WANAFUNZI wa kike wametakiwa kuongeza bidii katika masomo ya sayansi ili waweze kulisaidia Taifa katika kukabiliana na baadhi ya changamoto hususani katika sekta ya afya.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya wakati wa Mahafali ya Nne ya Shule ya Sekondari ya Wama Nakayama iliyopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Katika Mahafali hayo, Mhe. Mhandisi Manyanya amewapongeza wahitimu wote na kuwaeleza kuwa, masomo yote yana umuhimu sawa lakini pale wapatapo fursa wasome kwa bidii masomo ya Sayansi kwani kwa sasa kuna changamoto mbalimbali zinazozikabili Taifa hususani katika sekta ya afya ambapo endapo mkazo ukitiliwa basi utasaidia kutatua baadhi ya changamoto hizo kama vile upungufu wa Wataalam wa masuala ya afya na hivyo kuweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Alisema kuwa, Serikali kwa sasa inajitahidi kuangalia maeneo yenye upungufu wa Wataalam mbalimbali ili iweze kutatua changamoto mbalimbali ambapo elimu bora inahitajika katika kuwapata wataalam watakaoweza kutatua mapungufu hayo ndiyo maana inajitahidi kutoa elimu bure kwa sasa na kuendelea kuhimiza wanafunzi kusoma kwa bidii hasa wasichana ili elimu itolewayo iwe sawa kwa wote pasipo ubaguzi na kuweza kumkomboa msichana.
“Pale mpatapo nafasi ya kusoma, jitahidini musome masomo ya sayansi kwasababu kwa sasa masomo hayo yana nafasi kubwa na ajira yake ni ya uhakika na hata katika upatikanaji wa Vyuo Vikuu wakati wa kuomba unakuwa ni rahisi lakini pia mkiyapenda masomo haya mtakuwa wataalam ambao mtalisaidia Taifa letu katika kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali kama vile vifo vya akina mama na watoto, msife moyo kwa kuona kuwa ni magumu, someni kwa bidi siku zote”, alisema Mhandisi Manyanya.
Kwa upande wake Spika Mstaafu wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Spika Anne Makinda amewataka wahitimu hao kutobabaishwa na wanaume ambao wanaweza kuwadanganya kwa kuwarubuni kwa pesa na vitu mbalimbali na kuwataka kutokubali kwa namna yoyote ile.
“Mkombozi wa Mwanamke ni elimu, mkisoma kwa bidii hata hakuna mwanaume atakayewachezea ama kuwababaisha kwa pesa au vitu alivyonavyo, hivyo msikubali kudanganyika”, alisema Mhe. Makinda.
Naye Mwenyekiti wa Shule hiyo ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete alisema kwamba, anajivunia maendeleo makubwa yaliyopigwa na yanayoendelea kupigwa katika shule hiyo na ni kwa mara ya nne kwa wanafunzi wa kidato cha nne kuhitimu katika shule hiyo huku akiwataka wahitimu kuyafanyia kazi yale yote mazuri waliyojifunza wakati wa masomo yao.
Ameipongeza Serikali kwa ushirikiano mkubwa iliyoutoa kwa wanafunzi na pia wadau mbalimbali waliojitoa kwa moyo katika kusaidia uwepo wa shule hiyo lakini pia amewapongeza Walimu na wafanyakazi na wanafunzi wote kwa ujumla kwa kazi nzuri iliyofanikisha kung’ara kwa shule hiyo katika taaluma hususani katika Wilaya ya Rufiji.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Mwajuma Buguji alisema kwamba shule hiyo inapokea wanafunzi wa kike toka Wilaya na Mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na Visiwani ambapo wanafunzi wamegawanyika katika makundi mawili, wenye wazazi wote wawili ambao maisha yao duni, wenye wazazi mmoja na maisha yao ni duni na wengine ni yatima ambao maisha yao ni hatarishi.
Aidha, alisema kwamba wanafunzi hao kwa sasa wanapata ufadhili mkubwa toka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambapo hapo awali katika miaka ya nyuma baadhi ya wanafunzi waliojiunga na shule hiyo walichangia kiasi kidogo.
“Kwa sasa shule yetu ina jumla ya wanafunzi 378 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na leo wanahitimu wanafunzi 79, tunao wafanyakazi Walimu 26 na wasiokuwa walimu 13 na shule yetu inapiga hatua nzuri kimasomo kwa kuongoza Kiwilaya na kuchukua nafasi nzuri Kitaifa, alisema Mwl. Mwajuma.
Shule ya Wama Nakayama ilianzishwa mwaka 2010 na shule hiyo imetokana na majina mawili yaani WAMA pamoja na NAKAYAMA ambapo neno WAMA linasimama kama Taasisi ya Wanawake na Maendeleo na NAKAYAMA linasimama kama jina la mdau wa kwanza kuisaidia shule hiyo kwa kutoa msaada wa ujenzi ambaye ni Mfanyabiashara mkubwa toka nchi ya Japan.

ZIARA YA MAKONDA KINONDONI JANA.


ZIARA YA MAKONDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KINONDONI YANOGA LEO, AKATIZA VICHOCHORO KUSAKA KERO, ACHAPA KAZI KIKAMILIFU NA AFANDE SIRRO, AMTUMBUA MGANGA MKUU
 TUCHAPE KAZI KIONGOZI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwaga kicheko na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mkoa huo, walipokuwa wkijadili jambo, baada ya kuzungumza na viongozi na watendaji kutoka wilaya ya Kinondoni, katika Bwalo na Maofisa wa Polisi, Msaki mwanzoni mwa ziara yake katika mkoa wa Dar es Salaam, jana. Zifuatazo ni taswira katika picha kama alivyowanasa Mmiliki wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo aliyekuwa katika ziara hiyo.
  
 
 TANDALE
🔻
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua chumba cha biashara cha Mamalishe (kushoto), aliyemkuta akiwa kazini eneo la Tandale, akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Makonda akimwangalia mamalishe huyo wakati akiandaa chakula 
 Makonda na msafara wake wakikatiza mitaa ya Tandale wakati akisaka kero za wananchi wakati wa ziara hiyo ya aina yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wanne ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
 Salum Ali Hapi akimpa maelezo Makonda walipofika kukagua eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo Tandale, Kata ya Manzese
 Makonda akizungumza na wateja wa pombe za kieyeji aliowakuta katika kwenye kilabu cha pombe hizo, eneo la Uwanja wa Fisi
Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Mandela akikata funda la pombe ya kienyeji mbele ya Makonda bila wasiwasi kuwa yupo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  
 Makonda akijaribu kupiga hodi kwenye moja vya vyumba inayoelezwa kuwa ni ya madanguro ya ukahaba katika eneo hilo la Uwanja wa Fisi. Pamoja naye ni Hapi na Sirro 
 Kamanda Sirro naye akijaribu kumsaidia Makonda kupisha hodi lakini pia bila mafanikio ya kuitikiwa na waliokuwa wamejifungia ndani 
 Makonda akichukua bia kutoka kwa mhudumu wa baa pekee aliyoikuta wazi wakati myinge zote zikiwa zimefungwa kuhofia ujio wake.
 Makonda akiitazama kwa makini bia hiyo kuona tarehe yake ya mwisho wa matumizi, ili kujiridhisha kwa kuwa huelezwa kwamba baa zilizopo eneo hilo la Uwanja wa Fisi huuza vinywaji hadi vilivyokwisha mda wake wa matumizi. Bia hiyo aliikuta bado inafaa kwa matumizi.

 SHULE
 Makonda akitazama paa la chumba cha darasa katika shule ya Msingi Tandale, lililoporomoka wakati wa upepo mkali ulioambatana na mvua

MIUNDOMBINU YA BARABARA
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitazama majitaka yakitiririka kwenye daraja la barabara kutoka Tandale kwenda Mwananyamala. Makonda aliahidi barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami, la kwamba kabla ya hatua hiyo itafanyiwa matengenezo ya awali kuziba makorogoro ili iweze kupitika. 
 Makonda akipita pembeni pembeni kukwema maji machafu yaliyotuama kwenye sehemu ya barabara hiyo
 Mara huyu mama naye akamvaa na kumweleza kero zake wakati akipita


MKUTANO UWANJA WA SHULE YA MSINGI TANDALE
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi akimkaribisha Makonda kuanza kuunguruma ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu papo hapo au baadae, katika mkutano wa hadhara uliofayika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale, leo
 Makonda akizungumza 
 Makonda akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.
 Umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifuatilia jambo kwenye simu yake wakati wa mkutano huo. Mpogolo ni miongoni mwa waratibu wa ziara hiyo ya siku kumi ya Makonda katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.
 Watu wa huduma ya kwanza wakimpeleka kwenye gari ili kupelekwa haraka hospitali baada ya kuangua wakati wa mkutano huo
 Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa la Manispaa ya Kinondoni
 Wananchi kwenye mkutano huo
 Makonda akianza kujibu kero kwa kuwahoji watendaji kulingana na wananchi walivyotaka kujibiwa kero husika.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya (aliyeshika kinasa sauti), akisubiri hukumu ya Makonda baada ya kushindwa kueleza ikiwa alikuwa anajua au hajui kadhia ya dawa kuibwa mara kwa mara katika Zahanati ya Tandale kama wananchi walivyolalamika, ambapo alisema hajui
” Haiwezekani uwe Mganga Mkuu wa Wilaya katika mkoa wangu halafu hujui kuhusu kuibwa kwa dawa kwenye zahanati, hii haikubaliki, kuanzia sasa si mganga Mkuu wa Kinondoni, Nitawaambia wizara inayokuhusu wakupangine wilaya katika mikoa mingine ambako watavumilia uzembe kama papo”, alisema Makonda wakati akimtumbua Msuya kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika shule ya Msingi Tandale. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- theNkoromo Blog